Meneja Wa Makampuni
JF-Expert Member
- Jul 7, 2020
- 7,899
- 10,415
- Thread starter
- #21
Barua ya wazi wa Waziri wa Kilimo: Matumizi ya gesi asilia kuzalishia mbolea za kilimo (UREA, NA, CAN, SA, PA, CAN, MAPS na DAP).
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wakiagiza nje wanapiga dili vizuriNdugu mleta mada yule profesa sidhani kama hajui kitu kama hiko ulicho wasilisha hapa. Wanajua sana ila sijui nini kinacho wapelekea kuwa wazito katika kutekeleza mambo ambayo kwa namna moja ama nyingine yatainua hali ya taifa na wananchi moja kwa moja.
Inabidi wabadirike sasa, maana kipindi hichi ambacho gesi na mafuta vimekua ghali hata bei za mbolea zitakua ghali.Wakiagiza nje wanapiga dili vizuri
Yaani wabadilike waache kupata faida na familia zao wakujali wewe?Inabidi wabadirike sasa, maana kipindi hichi ambacho gesi na mafuta vimekua ghali hata bei za mbolea zitakua ghali.
Bei hizi zinakwenda kuwaumbua 😀😀😀😀😀Yaani wabadilike waache kupata faida na familia zao wakujali wewe?
Utaumbuka wewe na familia yako maana wao wanapewa bure kila kituBei hizi zinakwenda kuwaumbua 😀😀😀😀😀
Kenya wanaitoa wapi nduguKwa mfano kwa sasa hivi nimefatilia issue ya mbolea Rombo na Moshi Vijijini hadi Siha mbolea inachukuliwa Kenya kwa wingi sana na hawazalishi.
Kwako Mheshimiwa waziri wa kilimo,
Natumai ni mzima wa afya njema.
Mheshimiwa waziri wa Kilimo,
Rejea kichwa cha barua hii ya wazi kama kilivyo jieleza.
Naomba kurejea tena.
Matumizi ya gesi asilia kuzalishia mbolea za kilimo (UREA, Ammonium Nitrate (NA), Ammonium Sulphate (SA), Ammonium Phosphate (PA), Calcium Ammonium Nitrate (CAN), Monoammonium Phosphate (MAP), na Diammonium Phosphate (DAP)).
Mheshimiwa waziri,
Gesi asilia ndio malighafi kuu inayotumika kuzalishia mbolea zote zenye ubora zitumikazo kwenye kilimo hapa duniani.
Mataifa yote yanayotuuzia mbolea hapa Tanzania yanazalisha hiyo mbolea kwa kutumia gesi asilia.
Mheshimiwa waziri,
Tanzania ni nchi pekee Afrika mashariki iliyojaliwa kwa uwepo wa gesi asilia yenye futi za ujazo trillioni 57.54. Ni jambo la kumshukuru Mungu sana kwa neema hiyo. Lakini pamoja na neema hiyo bado gesi asilia haitumiwi ipasavyo katika taifa letu ili kuweza kuwaletea maendeleo watanzania.
Naweza kusema kwa sasa gesi asilia inatumika kuzalisha umeme. Ambapo asilimia 62 ya umeme unaozalishwa Tanzania unatokana na gesi. Unaweza kuona jinsi gesi ilivyookoa punguza mgao wa umeme katika sekta ya nishati ambao tuliupata miaka ya nyuma kipindi tunazalisha umeme kwa kutumia majenerata yanayotumia mafuta. Serikali imeokoa fedha nyingi ambazo zilitumika kuagiza mafuta kutoka nje ya nchi. Lakini pia gesi inatumika kwenye badhi ya vyombo vya moto na mashine na kupikia. Hapa naweza kusema wizara ya nishati iliionyesha uthubutu mkubwa kuingiza gesi asilia katika sekta hii ya nishati.
Mheshimiwa waziri wa kilimo, kama nilivyo ainisha faida tulizozipata kutoka kwenye gesi asilia hapo juu, naweza kusema tena kuwa gesi asilia inamatumizi mengi. Mataifa makubwa duniani yanatumia fursa hiyo kuzalisha bidhaa mbalimbali kwa kutokana na gesi. Mbali ya kupikia, kuwashia, kuzalishia umeme, kutumika viwandani na kutumika kwenye magari na machine zingine mbalimbali. Gesi asilia ni kemikali nzuri sana inayotumika kuzalishia mbolea. Mbolea zote zinazozalishwa Urusi, Ukraine, Qatar na mataifa mengine duniani zinatokana na gesi asilia, ndio malighafi na ndio mbolea zenye ubora katika kuzalisha mazao ya kilimo.
Mheshimiwa waziri,
Kilimo ndio uti wa mgongo wa taifa la Tanzania. Watanzania wanategemea kilimo ili waweze kujiendesha kimaisha. Kilimo kimeajiri idadi kubwa ya watanzania na maisha yanaendelea, ila tatizo la mbolea limeendelea kuongezeka Tanzania. Watanzania wanategemea mbolea ili waweze kulima kilimo bora kinachotoa mazao bora. Lakini mheshimiwa waziri mbolea bado ni tatizo. Mimi kama mkulima naweza kusema tatizo la mbolea Tanzania linatatulika, na nitaeleza tufanyeje ili tuweze kutatua tatizo hili lakini in long term.
Ndugu Mheshimiwa waziri, Mimi naona dawa pekee ya kutatua tatizo la mbolea nchini Tanzania ni kujenga kiwanda cha mbolea bora zinazozalishwa kwa kutumia gesi asilia. Hizo ndio mbolea zenye nguvu ya kutoa virutubisho vya kutosha kwenye mimea. Na ndio sababu unaona mbali na kwamba tuna kiwanda cha mbolea Tanzania lakini bado huwa tunaagiza mbolea kutoka mataifa ya nje. Sio kwamba tu ni kwasababu mbolea inayozalishwa ndani haitoshelezi lahasha hata ubora wa mbolea yenyewe hautoshelezi kuzalisha mazao bora na mengi.
Ndugu Mheshimiwa waziri analysis za kujenga kiwanda cha mbolea Lindi zilishafanywa, na wawekezaji walijitokeza wakakubali kujenga kiwanda cha kuzalisha mbolea Tanzania. Na kwakua wateja wapo mimi naona huo mradi utaweza kuleta faida. Mheshimiwa waziri hili ni jambo la neema sana endapo ukilipa kipaumbele zaidi katika wizara yako ya kilimo.
Ndugu mheshimiwa waziri,
Naomba niweze kuelezea kidogo jinsi ambavyo gesi asilia itaweza kubadilishwa kuwa mbolea kama kichwa kinavyo jieleza hapa chini.
KUIBADILI GESI ASILIA KUWA MBOLEA ZA KILIMO KUTAINUA UCHUMI WA TANZANIA.
MBOLEA zinazotumika kwenye kilimo huzalishwa kwa kuibadili GESI ASILIA katika nchi zilizo endelea. Kilimo kinaweza kutufaidisha kama tukianzisha kiwanda cha kubadilisha GESI ASILIA kuwa MBOLEA nchini.
Tanzania huaagiza 90% ya mbolea kutoka nje, 10% huzalishwa ndani.
1/4 ya Uchumi wetu hutegemea kilimo. Kinatoa 85% ya bidhaa zinazouzwa nje ya nchi na kinaajiri 80% ya watanzania.
Tukianzisha kiwanda cha kuzalisha tani 2300 za AMMONIA na tani 4000 za UREA kwa siku (tani Millioni 1.3 za urea kwa mwaka), tutakidhi mahitaji ya ndani na kiasi cha mbolea inayobaki kikauzwa nje ya nchi.
Hatua za kubadilisha GESI ASILIA kuwa MBOLEA.
1. GESI ASILIA (CH4) itabadilishwa kuwa AMMONIA kwa miungano ya kikemikali. AMMONIA yenyewe ni mbolea tayari.
2. AMMONIA itabadirishwa kuwa UREA kwa kutumia miungano ya kikekimali.
Lakini pia kutoka kwenye AMMONIA tutafanya miungano mingine ya kikemikali kupata mbolea za; AMMONIUM NITRATE (NA), AMMONIUM SULPHATE (SA), AMMONIUM PHOSPHATE (PA).
Kutoka kwenye AMMONIUM NITRATE (NA) tutapata mbolea ya CALCIUM AMMONIUM NITRATE (CAN). Kutoka kwenye AMMONIUM PHOSPHATE (PA) tutapata mbolea ya MONOAMMONIUM PHOSPHATE (MAP), na DIAMMONIUM PHOSPHATE (DAP).
Mheshimiwa waziri nichukue fursa hii kukushukuru kwa dhati kwa kuisoma barua yangu.
Ahsante.
Haya tunayo yaandika yatasomwa na vizazi vijavyo hata yasipofanyiwa kazi leo hii ni bora tuendelee kuandika ndio kazi tuliyopangiwa kuandika kushauri na kusema ukweli.Kuna mambo ukiyasema Serikali ni sawa unashika sharubu za simba na kuzichezea.
Wengi was viongozi was serikali ni mental slave thinkers. Wanafikiria kujikimbikizia. Na ktk mbolea ni sehemu moja yapo ya kuchota mapesa kwa ajili ya wao na watoto wao. Chukulia anaambiwa atapata sh 1 kwa tani za mbolea akiidhisha kuuzwa tz.
Sasa ndugu yangu ungemaliza kwa kuweka link za mini plan za mbolea tujue zinauzwajwe. Ili bei zikiwa rafiki sisi kazi yetu iwe kuhamasisha wanunuee ña kuzalisha.
Hakuna namna.
from China Manufacturer. | Made-in-China.com Mobile
China , offered by China manufacturer & supplier -m.made-in-china.com
Ni kweli na ni bora tuandike jambo ili ije kusomwa kama sehemu ya historia. Badala ya kuandika ushauri usiokamilika. Ushauri, onyesha njia na kufanya uchambuzi was gharama. Mini bora, kutengeza au kununua. Kwa References zipiHaya tunayo yaandika yatasomwa na vizazi vijavyo hata yasipofanyiwa kazi leo hii ni bora tuendelee kuandika ndio kazi tuliyopangiwa kuandika kushauri na kusema ukweli.
Kawaulize EU wamesemaje kuhusu mbolea. Umoja wa ulaya wamekataza kununua mbolea wametutaka tutengeneze mbolea za kwetu.Ni kweli na ni bora tuandike jambo ili ije kusomwa kama sehemu ya historia. Badala ya kuandika ushauri usiokamilika. Ushauri, onyesha njia na kufanya uchambuzi was gharama. Mini bora, kutengeza au kununua. Kwa References zipi
Tukiacha hizi harakati ukipata fursa ya kutafuta masoko ya mbolea utaiweza kazi hii. How. NikutonyeKawaulize EU wamesemaje kuhusu mbolea. Umoja wa ulaya wamekataza kununua mbolea wametutaka tutengeneze mbolea za kwetu.
Ndugu hizo ni kampaundi za kikemikali zenye uwezo wa kutoa madini ya kurutubisha mimea. Hizo kampaundi zimeundwa kwa element.Kuna yyt anaeweza kunifafanulia kwa lugha rahisi tofauti ya haya maneno(UREA, NA, CAN, SA, PA, CAN, MAPS na DAP)
Na je soko la mbolea liko vipi, ikiletwa brand mpya vipi yaweza kukamata soko.
Maana hakuna namna.
Masoko ya namna gani unataka.Tukiacha hizi harakati ukipata fursa ya kutafuta masoko ya mbolea utaiweza kazi hii. How. Nikutonye