Ryzen
JF-Expert Member
- Dec 6, 2012
- 7,301
- 8,706
Nilianza kuishabikia mwaka 2005 kwa ushabiki wangu kwa Ronaldinho Gaucho! Ni club ambayo hata kama nina stress inaweza kunifurahisha na kuniondolea stress zangu.....Katika vitu vitatu Muhimu ninavyovipenda na Club yangu ya FC Barcelona ipo!
Tumekuwa Club inayotisha kwa kutengeneza Dream team kuanzia kwa Kina Josep Guardiola, Ronald Koeman mpaka kizazi cha Xavi Hernandez, Lionel Messi Cucitini, Andres Iniesta na Sergio Busquets, Kiufupi kwa Miaka Karibu kumi iliyopita FC BARCELONA ndio ilikuwa Club Bora Duniani!
Lakini nini nia ya kuandika Barua Hii? Nia ya kuandika Barua Hii ni kuukumbusha Menejimenti yetu pamoja na raisi Bartomeu kwamba tumejisahau tukiamini kizazi cha kina messi na iniesta hakitopita, Hamtafuti mbadala wa hawa viumbe ambao wanaelekea ukingoni mwa soka lao, Tizama mpaka leo hakuna alieziba nafasi ya Xavi kikamilifu!
Tunazidi kuwapa nafasi wapinzani wetu Real Madrid kutuzidi kila idara kwa mfano kwa miaka Mingi Kiungo wetu FC Barcelona ndo ilikuwa kiungo Hatari zaidi Duniani sasa hiyo Nafasi imehamia kwa Wapinzani wetu wakubwa Huku sisi tukiwa tumezubaa...Tizama wamemsajili Theo Hernandez, Dani Ceballos na wengine Huku sisi tukiwa hatujasajili hata mmoja!
eti klabu inan'ga'gana na Paulinho embu acheni mchezo mwageni kitita chochote cha Pesa tumpate Marco Verrati na Bellerin Hapo Angalau Roho zetu Mashabiki zitatulia!
Kwa Leo Barua yangu inaishia Hapa
Ni mimi Mshabiki wenu wa Damu TheMason