Barua yangu ya wazi kwa klabu yangu FC Barcelona!

Barua yangu ya wazi kwa klabu yangu FC Barcelona!

Ryzen

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2012
Posts
7,301
Reaction score
8,706
1200px-FC_Barcelona_%28crest%29.svg.png

Nilianza kuishabikia mwaka 2005 kwa ushabiki wangu kwa Ronaldinho Gaucho! Ni club ambayo hata kama nina stress inaweza kunifurahisha na kuniondolea stress zangu.....Katika vitu vitatu Muhimu ninavyovipenda na Club yangu ya FC Barcelona ipo!
Tumekuwa Club inayotisha kwa kutengeneza Dream team kuanzia kwa Kina Josep Guardiola, Ronald Koeman mpaka kizazi cha Xavi Hernandez, Lionel Messi Cucitini, Andres Iniesta na Sergio Busquets, Kiufupi kwa Miaka Karibu kumi iliyopita FC BARCELONA ndio ilikuwa Club Bora Duniani!

Lakini nini nia ya kuandika Barua Hii? Nia ya kuandika Barua Hii ni kuukumbusha Menejimenti yetu pamoja na raisi Bartomeu kwamba tumejisahau tukiamini kizazi cha kina messi na iniesta hakitopita, Hamtafuti mbadala wa hawa viumbe ambao wanaelekea ukingoni mwa soka lao, Tizama mpaka leo hakuna alieziba nafasi ya Xavi kikamilifu!

Tunazidi kuwapa nafasi wapinzani wetu Real Madrid kutuzidi kila idara kwa mfano kwa miaka Mingi Kiungo wetu FC Barcelona ndo ilikuwa kiungo Hatari zaidi Duniani sasa hiyo Nafasi imehamia kwa Wapinzani wetu wakubwa Huku sisi tukiwa tumezubaa...Tizama wamemsajili Theo Hernandez, Dani Ceballos na wengine Huku sisi tukiwa hatujasajili hata mmoja!

eti klabu inan'ga'gana na Paulinho embu acheni mchezo mwageni kitita chochote cha Pesa tumpate Marco Verrati na Bellerin Hapo Angalau Roho zetu Mashabiki zitatulia!
Kwa Leo Barua yangu inaishia Hapa

Ni mimi Mshabiki wenu wa Damu TheMason
 
Jombaa, kule ulaya sio sawa na hapo sokoni ilipo Simba. Hakuna ushabiki wa damu wala makamasi, we cha msingi hapo kwenye barua yako chini andika namba yako ya uanachama na sio porojo.
 
Mkuu TheMason pole sana kwa uchungu unaokupata but me nakushauri reserve your words season ya kusajili bado haijafungwa na team ina kocha mpya yapo mazuri mengi sana yanakuja ,kama team ime make sana profit kwa kutumia hao wachezaji wa golden age ya Barcelona lakini nakulazimisha uamini still Golden age ya Barca(facts zangu zina rely kwenye statistics na sio emotions ) bado inaendelea
Trust me
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Mkuu Barcelona wapo humu ndani nadhan barua yako wataiona

Sent from my SM-N910C using JamiiForums mobile app
 
Kwani hicho kitita hakikupelekwa kwa verratti?

Sent from my IK-644 using JamiiForums mobile app
 
OMBI LAKO UONGOZI WA FC BARCELONA WATALIFANYIA KAZI ILA NIKUPE UHALISIA KUWA BARCELONA HAIWEZI KUKUANGUSHA NA HAITOKAA ITUANGUSHE BADO TUNA IMANI NA BARCELONA TIMU BORA KULIKO ZOTE ULIMWENGUNI
 
Uongozi its not black and white decisions kama colour tunaweza sema ni grey,sidhani kama Bartmeo &BOD wanashindwa kusajili ila inatokana na mahitaji ya coach Velverde ni type ya makocha ambao ni wafuasi wa tick taka kutoka kwa mwl wake founder Johan Cruyff anashinda mchezo na hata mediocre players kwa sababu wanaamini inayocheza ni team yote kuanzia kwa goalkeeper hadi 11(chain playing)
Lets see team yetu kwenye preseason wanachezaje na BOD ita respond pia
 
1200px-FC_Barcelona_%28crest%29.svg.png

Nilianza kuishabikia mwaka 2005 kwa ushabiki wangu kwa Ronaldinho Gaucho! Ni club ambayo hata kama nina stress inaweza kunifurahisha na kuniondolea stress zangu.....Katika vitu vitatu Muhimu ninavyovipenda na Club yangu ya FC Barcelona ipo!
Tumekuwa Club inayotisha kwa kutengeneza Dream team kuanzia kwa Kina Josep Guardiola, Ronald Koeman mpaka kizazi cha Xavi Hernandez, Lionel Messi Cucitini, Andres Iniesta na Sergio Busquets, Kiufupi kwa Miaka Karibu kumi iliyopita FC BARCELONA ndio ilikuwa Club Bora Duniani!

Lakini nini nia ya kuandika Barua Hii? Nia ya kuandika Barua Hii ni kuukumbusha Menejimenti yetu pamoja na raisi Bartomeu kwamba tumejisahau tukiamini kizazi cha kina messi na iniesta hakitopita, Hamtafuti mbadala wa hawa viumbe ambao wanaelekea ukingoni mwa soka lao, Tizama mpaka leo hakuna alieziba nafasi ya Xavi kikamilifu!

Tunazidi kuwapa nafasi wapinzani wetu Real Madrid kutuzidi kila idara kwa mfano kwa miaka Mingi Kiungo wetu FC Barcelona ndo ilikuwa kiungo Hatari zaidi Duniani sasa hiyo Nafasi imehamia kwa Wapinzani wetu wakubwa Huku sisi tukiwa tumezubaa...Tizama wamemsajili Theo Hernandez, Dani Ceballos na wengine Huku sisi tukiwa hatujasajili hata mmoja!

eti klabu inan'ga'gana na Paulinho embu acheni mchezo mwageni kitita chochote cha Pesa tumpate Marco Verrati na Bellerin Hapo Angalau Roho zetu Mashabiki zitatulia!
Kwa Leo Barua yangu inaishia Hapa

Ni mimi Mshabiki wenu wa Damu TheMason
Tulia mkuu. Kimsingi Mungu aliumba vitu viwili viwili na kwa mambo haya ni suala la kupisha muda tu huku tukipanga mipango mipya. Timu nyingi sasa hivi tukikutana nazo hupambana vilivo kuliko wakutanapo na Real Madrid kwa maana aina yetu ya uchezaji mpira wa kistaarabu kwao wao wanaamua kutumia miguvu na kujihami vilivo. Waswahili husema 'ukimuona kobe kainama, ujue anatunga sheria', Barca halisi anaamini huu ni upepo unapita na muda ukifika tutarejea kileleni. Kwa sasa bado wachezaji wetu wapo katika kiwango cha hali ya juu na kumbuka kushuka kiwango kwa timu yetu hata timu yao ya taifa imeshuka vilevile.
 
OMBI LAKO UONGOZI WA FC BARCELONA WATALIFANYIA KAZI ILA NIKUPE UHALISIA KUWA BARCELONA HAIWEZI KUKUANGUSHA NA HAITOKAA ITUANGUSHE BADO TUNA IMANI NA BARCELONA TIMU BORA KULIKO ZOTE ULIMWENGUNI
Barca Barca Baaaaaaaaaaaaaaaaarca!
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Kumbe Barcelona wapo jf. Ok sawa!
 
Eti shabiki wa Barca, huna membership card, huna hata jezi original ya Barca, unashinda kinesi unalinganisha na La Masia, wewe ni mfuasi tu.
 
Replacement ya Xavi, Iniesta hamtokuja ipata siku za karibuni. Messi ndo kabisaa, hatokuja patikana miaka ya karibuni.

Madrid ilituchukua miaka toka kizazi cha wakina Guti, Morientes, Raul, Solari, Redondo, Hiero kiondoke. Hata hivyo nasema tuu kuwa, bado timu haijawa njema sana kama kipindi kile. Casemiro anajaribu tuu kuvaa viatu vya makelele, Toni kroos anamiss vitu vya Jose maria Guti, Benzema hana vitu vya Morientes, ila ndo timu inayosumbua sasa hivi.

By the way, mlifanya makosa kutokumuamini Fabregas, huyu ndo alikuwa perfect replacement ya iniesta, pia ilikuwa ni mistake kumuachia Alcanthara.

Ila pamoja na yote, Madrid tunaitamani sana foward line yenu. Hebu fikiria tungekuwa na foward kama suarez mbadala wa Benzema, Neymar mbadala wa Bale tungekuwaje.?

Yote kwa yote, huwezi pewa vyote.
 
Back
Top Bottom