Action and Reaction
JF-Expert Member
- Oct 16, 2021
- 1,438
- 1,496
Wanajamii wenzangu, barua yangu ya uhamisho katika ngazi za wilaya ilikamika kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine baada ya kusota kwa muda mrefu na nilishapeleka mkoani.
Nashindwa kuelewa process ya mkoani kwenda wizara itachukua muda gani isije ikawa zinawekwa kapuni mana mpaka naifikisha mkoani daaa ni Mungu pekee maana rushwa nilishakataaga nafsini mwangu!
Wengine wanahama ndani ya mwezi mmoja tangu waanze process ila mie msoto niliokula unatosha! Kuna jamaangu alitoa 2M ndani ya wiki mbili akahamishwa, akaniunganishia mchongo huo nikagoma aisee!
NB: Kuna ukweli kwamba huwa ni vipindi viwili mwezi wa 6 na wa 12? LAKINI kuna watu wanahama kabla ya wakati huo. So sielewi inakuwaje wanajamii!