Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Tanzania ni taifa ambalo katika miaka kadhaa nyuma lilikumbwa na mauaji makubwa ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) haswa kipindi cha uchaguzi kilipokuwa kinakaribia. Licha ya matukio hayo mwaka 2010, historia iliandikwa na Barwan Salum baada ya kuchaguliwa kuwa mbunge wa jimbo la Lindi, kusini mwa Tanzania na kuwa Mbunge pekee albino kuchaguliwa na wananchi nchini Tanzania na hata Afrika Mashariki.
Kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Novemba 27 Mwenyekiti wa CHADEMA, Lindi mjini Barwan Salum amewataka watu wa karibu wahamasishe watu wenye ulemavu kuwania nafasi za uongozi kwasababu ni sehemu ya Jamii ambayo inatakiwa kunufaika na nafasi hizo.
Soma, Pia: