maroon7
JF-Expert Member
- Nov 3, 2010
- 11,311
- 15,640
Katika vitu vya kushangaza ni hili la msanii harmonize kutaja matusi kwa makusudi tena kwa kurudiarudia bila ya kujali uwepo wa viongozi wa nchi siku ile ya yanga day.
Nilitegemea angenyang'anywa kipaza sauti na waandaaji lakini ajabu haikua hivyo. Akaendelea tena na tena kutamka lile neno bomboclat qmbalo ni tusi kubwa lenye kufedhehesha linalotumika Jamaica. Ikumbukwe pia nchi nzima akiwemo Rais wa nchi walikua wakitazama matangazo yale moja kwa moja.
Inachoshangaza zaidi ni BASATA kulikalia kimya kabisa kana kwamba ni kitu cha kawaida kilichotokea, sasa sielewi ni sababu hawaelewi maana ya bomboclat au wanahisi watu hawaelewi maana yake hivyo wamepotezea.
Kuonesha kuwa haikua bahati mbaya kwa harmonize kutukana kwa kurudiarudia,alidiriki hata kuongea upuuzi kwa kutamka kupenda wanawake wenye makalio makubwa..huku akijua pale sio club na watu wa rika zote wanatazama yale matangazo. Hivi hawa BASATA wanajielewa kweli?