BASATA Hongereni Kumfungia Diamond na Tabia Zake za Hovyo Zisizovumilika

chotera

JF-Expert Member
Joined
May 19, 2016
Posts
6,560
Reaction score
15,864
Kwanza Nilikua najiuliza huyu dogo mambo yote ya hovyo anafanya na kusamehewa lakini bado mnambeba tu?
Mbona wasanii wengine hawafanyi ujinga kuanzia maisha halisi hadi kwenye mitandao ya kijamii?
Mlichofanya mnastahili pongezi kwani mnasimamia maadili na ukiangalia nyimbo zote za huyu msanii wa hovyohovyo kitabia ni mbovu tu maadili hazina Watanzania tujifunze kussuport watu wanaojiheshimu kwenye jamii.
 
Sasa akifungiwa mtoto wako atasoma wapi?, unajua kwamba diamond analipa kodi kupitia muziki?
 
Anachokifanya Diamond ni mashart ya mganga from Hollywood.....kutoka kule ili ufanikiwe katika tasnia ya burdan lazima uhamasishe moja wapo ya hv vtu vtatu.1.Ngono 2.Uchawi. 3.Mauaji...angalia filamu zote duniani, na miziki yote lazima ihamasishe kimoja wapo...
 
Kaanza kufanikiwa kabla "hajahamasisha" hayo unayoyasema
 
BASATA nilikuwa nawashangaa huu uchafu unamwagwa na huyu kijana aliyekosa maadili na nyie mnamlea tu. Na wengine pia fuatilia aibu kwa Taifa lililoheshimika wakati wa Nyerere
 
BASATA nilikuwa nawashangaa huu uchafu unamwagwa na huyu kijana aliyekosa maadili na nyie mnamlea tu. Na wengine pia fuatilia aibu kwa Taifa lililoheshimika wakati wa Nyerere
Tuna Raisi mwenye msimamo imara asiyeyumbishwa ,fanyeni kazi kwa mfano wake mzuri; amewaweka ili mnyooshe mambo kwa niaba yake. Ziko nyimbo nyingi chafu zimezagaa kila mahali fuatilieni muokoe watoto wetu
 

kweli hata mtaani kwenu una karoho kwa kuona watu wanishindwa
 
Huwezi kustruggle kwa kufanya uchafu, ni kama shoga aseme anstruggle. Tuache u-zezeta
Hakuna uzezeta hapo....ni utaratibu tu wa kazi.... akiimba tofaut lazma atashuka..we ndo zezeta kwa sababu hujui
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…