BASATA: Tulimzuia Nay wa Mitego kufanya shoo kwa kuwa amekataa wito wetu mara mbili

BASATA: Tulimzuia Nay wa Mitego kufanya shoo kwa kuwa amekataa wito wetu mara mbili


Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limesema limetoa wito mara mbili kwa Msanii wa Bongo Fleva, Nay wa Mitego kufika ofisini kwa ajili ya mazungumzo khusu wimbo wake wa Amkeni lakini hakutokea na hiyo ndio sababu ya taasisi hiyo kumnyima vibali vya kufanya shoo Mkoani Njombe.

Mwanasheria wa BASATA, Christopher Kamgisha amesema “Tumempa wito kwa mara ya tatu afike Ijumaa hii (Septemba 8, 2023), masuala ya Polisi hatuyajui, sisi tunadili na maadili ya Msanii.

Awali, Mwanasheria wa Nay, Wakili Jebra Kambole alisema “BASATA wamempa wito wa maandishi Nay kuwa aende ofisini kwao Ijumaa hii kwa sharti anatakiwa kwenda peke yake bila Mwanasheria, bado tunatafakari sharti hilo kama aende mwenyewe au la na kwa nini iwe hivyo.”

Pia soma - Msanii Nay wa Mitego ahojiwa na Polisi na kufunguliwa kesi ya Uchochezi
'Maadili ya msanii'!! Wengine nyimbo zao ni ngono mwanzo mwisho, wako salama! Hii Serikali , kuanzia rais ni mauzauza, maadili kwa rais anaona maaskofu hawatekelezi wajibu wao kwa usahihi, wakati yeye binafsi anazungurukwa na wasanii wanaoiharibu jamii kwa taswira na jumbe zao zilizokengeuka, hawaoni kwa sababu wanampa ulaji, upigaji.
 
Back
Top Bottom