PreGE2025 BASATA & Tume ya uchaguzi zuia tapeli Msama na tamasha lake la kuombea uchaguzi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Huihui2

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2012
Posts
9,818
Reaction score
14,585
Huyu tapeli ana rekodi mbaya kwenye utapeli wa ardhi na madawa ya kulevya. Nawasihi BASATA au Tume ya uchaguzi (NEC) msimruhusu kamwe ajihusishe na uchaguzi mkuu wa 2025.

--
TAMASHA la kuombea Uchaguzi Mkuu linatarajiwa kufanyika katika mikoa 26 ya Tanzania, likianza jijini Dar es Salaam mwaka huu.

Tamasha hilo litapambwa na waimbaji mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi, likiwa na lengo la kuhimiza amani na mshikamano kuelekea uchaguzi mkuu.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Machi 24, 2025, Mkurugenzi wa Msama Promotion, @alex_msama , amesema ibada hiyo ni sehemu ya maandalizi ya kuelekea uchaguzi mkuu wa madiwani, wabunge, na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

β€œLengo ni kuweka umoja na ushirikiano miongoni mwa Watanzania, kuwaombea viongozi watakaochaguliwa ili waweze kutuongoza kwa hekima na busara,” alisema Msama.

Tamasha hilo litashirikisha waimbaji kutoka Tanzania, Kenya, Uganda, na Rwanda, ambao wanatarajiwa kutoa burudani na kushiriki maombi maalum kwa ajili ya uchaguzi.

Aidha, Msama amewaomba viongozi wa vyama vya siasa kuhakikisha wanatumia lugha zenye heshima katika mikutano yao ya kampeni badala ya lugha za matusi, ili kuhimiza siasa safi na yenye maadili kwa vizazi vya sasa na vijavyo.

Pia, amewataka wadau na watu mbalimbali kujitokeza kutoa ushirikiano wa kudhamini tamasha hilo ili kuhakikisha linafanikiwa na kuleta ujumbe wa amani na mshikamano kwa Watanzania wote\

Your browser is not able to display this video.
 
Jamaa maisha yKe tu ni uzushi uzushi mwanzo mwisho
Huyu Ruge sjui alimuokota wapi bora angemuacha aendelee na udereva taxi tu mjini

Ova
 
Mzee wa fursa
 
Tatizo kubwa la watanzania wengi ukiwemo mtoa thread ni WIVU,CHUKI na ROHO MBAYA .
 
Siasa hasa siasa zakwenye uchaguzi na vyama ni fursa zakupiga ela kwa watu.kuna mwingine nilimuona anaratibu kikundi cha ngoma ili aje akitafutie tenda kipindi cha kampeni.Na mwaka huu ela iko nje nje.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…