PreGE2025 BASATA & Tume ya uchaguzi zuia tapeli Msama na tamasha lake la kuombea uchaguzi

PreGE2025 BASATA & Tume ya uchaguzi zuia tapeli Msama na tamasha lake la kuombea uchaguzi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Jamaa maisha yKe tu ni uzushi uzushi mwanzo mwisho
Huyu Ruge sjui alimuokota wapi bora angemuacha aendelee na udereva taxi tu mjini

Ova
Huyu alikuwa Taxi driver wakati Clouds inaanza. Kwa hiyo akawa anakodiwa sana na uongozi wa Clouds chini ya Ruge. Eventually kwa roho ya Ruge akamfungulia fursa. Hakujuwa kuwa ni muovu kiasi hiki
 
Huyu alikuwa Taxi driver wakati Clouds inaanza. Kwa hiyo akawa anakodiwa sana na uongozi wa Clouds chini ya Ruge. Eventually kwa roho ya Ruge akamfungulia fursa. Hakujuwa kuwa ni muovu kiasi hiki
Namjuwa vizuri sana huyu mzushi

Ova
 
Huyu TAPELI hachoki, leo amekuja kivingine:-
20250610_075052.jpg
 
This time Alex Msama ameingia "choo cha mashoga"


Screenshot_20260123_085022_Instagram.jpg
 
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imetangaza kuwatafuta washtakiwa Alex Msama Mwita na Benny Mwita Sammoh wanaokabiliwa na mashtaka ya uhujumu uchumi ikiwemo kuongoza genge la uhalifu, kughushi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu pamoja na utakatishaji fedha kupitia shauri la uhujumu uchumi Na. 1371/2026

Taarifa kwa umma iliyotolewa na Naibu Mkuu wa TAKUKURU (M) Kinondoni Elizabeth Mokiwa kupitia kwa Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam leo, Alhamisi Januari 22.2026 imebainisha kuwa shauri hilo limefunguliwa Januari 21.2026 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Hassan Makube, ambapo uwepo wa shauri hilo ni matokeo ya uchunguzi wa tuhuma kuhusiana na kiwanja Na. 33 kilichopo eneo la Vijibweni, Kigamboni, mkoani Dar es Salaam lenye hati Na. 129621 iliyotolewa kwa Africa Energy Limited mwaka 2013

TAKUKURU imesema washtakiwa hao wanadaiwa kughushi hati ya mauziano ya eneo husika na kuwasilisha kwenye Baraza la Ardhi la Wilaya ya Temeke ikionesha kuwa Benny Mwita Sammoh amenunua kiwanja hicho kutoka kwa Mwinyikombo Wahela huku wakijuwa kuwa sio kweli

Imeelezwa kuwa kufuatia wasilisho hilo kwenye Baraza la Ardhi la Wilaya ya Temeke, Benny Mwita Sammoh kwa kutumia jina lingine la Ben Samson alifanikiwa kuuza eneo hilo kwa kampuni ya World Oil Tanzania Limited na kujipatia jumla ya Tsh. 984,000,000/- kati ya Tsh. 1,700,000,000/- zilizoainishwa kwenye mkataba wa mauzo, ambapo ushahidi uliopatikana unaonesha kuwa Benny Mwita Sammoh alihamisha jumla ya Tsh. 370,000,000/- kati ya Tsh. 984,000,000/- kwenda kwa Alex Msama Mwita ikiwa ni sehemu ya fedha zilizotokana na mauzo ya kiwanja husika

Taarifa hiyo imeendelea kufafanua kuwa uchunguzi huo umefanywa na timu ya uchunguzi kutoka Ofisi za TAKUKURU Kinondoni na Temeke, ambapo baada ya kukamilika washtakiwa wote walitakiwa kuripoti Ofisi ya TAKUKURU Kinondoni Desemba 2025 ili wafikishwe Mahakamani jambo ambalo hawakulitekeleza

"Jitihada mbalimbali za kuwataka kufika zimefanyika bila mafanikio hivyo tunaomba mwananchi yeyote mwenye taarifa za upatikanaji wao kutoa taarifa kwenye Ofisi yoyote ya TAKUKURU au kupiga simu Na. 0738150236, zawadi nono itatolewa kwa atakayefanikisha, hati za kuwakamata zimeshatolewa na Mahakama ya Kisutu tarehe 21 Januari 2026 na shauri hili litatajwa tena tarehe 25 Februari 2026", imeeleza sehemu ya taarifa hiyo

Aidha, TAKUKURU imesema sambamba na mashtaka hayo Alex Msama Mwita anatafutwa pia na Ofisi yake ya Kinondoni kwa ajili ya kujibu tuhuma za kughushi na uvamizi wa eneo la kiwanja Na. 234 kilichopo Regent Estate Mikocheni, Wilaya ya Kinondoni, Mkoa wa Dar es Salaam

Kupitia taarifa hiyo, TAKUKURU imetoa tahadhari kwa watumishi wa umma kutoshiriki katika vitendo vya kufanikisha watu kujipatia umiliki wa viwanja kwa njia ya udanganyifu, hiyo imeenda sambamba na wananchi kutahadharishwa kupata taarifa sahihi kabla ya kufanya ununuzi wa viwanja hususani viwanja vilivyopo katika maeneo ya kimkakati.
 
Uzuri kwenye hili TAMASHA atatajwa Samia kila baada ya maneno matano. Kwasababu hiyo sahau ndoto yako ya kulifungia. Hukusikia jana akipinga Noreform No election? Akili kumkichwa ndugu yangu.
Inasikitisha sana
 
Back
Top Bottom