BASATA waufungia wimbo wa Nay 'Nitasema'

BASATA waufungia wimbo wa Nay 'Nitasema'

Kwani Msomi Mwana FA anasemaje?

Na Ney Wa Mitego angeandika "Njagu" badala ya "polisi" ingeeleweka.

Hivi hawezi kwenda mahakamani?
 
Sawa lakini ujumbe umewafikia na sisi tulisha ipata hiyo nyimbo ipo kwenye simu zetu na PC zetu 😎
 
Sasa wajameni mbona wabongo watu vituko,kwani zile nyimbo chafu chafu za milionea wenu mnayejivunia hamja ziona sembuse kuzisikia?Bongo lala tabu tabu tupu.
 
Hicho ndio kinanishangaza wabongo kweli tumekuwa wajinga wa viwango hivyo?
 
Huyu jamaa anahitaji support sana ya wabongo, nadhani ni msanii pekee ambaye ambaye kwake ishu za Kingono ambazo hata wanyama kama mbwa hufanya, yeye huongelea mambo ambayo ni daraja la la juu la binadam
 
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limeufungia rasmi wimbo 'Nitasema' wa msanii Nay wa Mitego kwa madai ya kukiuka Kanuni ya 25 ya baraza hilo. Katika barua rasmi iliyotolewa na BASATA, wimbo huo umeonekana kuwa na maneno yanayokiuka maadili ya jamii, ikiwemo "wanaokuja kututeka, wanakuja kama polisi" na "na mkikosea, tukikosa, mnatutumia polisi". Maneno haya yametajwa kama yenye ukakasi na kutokuwa na ushahidi wa kuthibitisha madai hayo, hivyo kusababisha kufungiwa kwa wimbo huo kwa mujibu wa kanuni husika.
IMG_0137.jpeg
Nay wa Mitego, kupitia akaunti yake ya Instagram, alijibu hatua hiyo kwa kusema kuwa vyombo vya habari nchini tayari vilikuwa havipigi nyimbo zake kutokana na kile alichokiita kuwa "chawa wa serikali." Nay alieleza kushangazwa na hatua ya kufungia wimbo ambao hata hivyo haukuwa unapigwa kwenye vyombo vya habari.

IMG_0138.jpeg
 
Wakuu,

Ila BASATA mmekuwa zaidi ya mizigo! Kwa hawa watu wote wanaotekwa na kuwataja polisi 🤣 🤣 au wenzetu hamjui Kiswahili. Mapana naona ndio utakuwa kiongozi kituko kuwahi kutokea tokea BASATA ianzishwe!

Halafu serikali na CCM hamjifunzi, yaani mnarudia mambo yale yale ambayo yakuja ku backfire, mnareact ovyo ovyo bila kujipanga. Mngeuchuna wala huu wimbo usingekuwa ishu, sasa mnafanya hata wale ambao hawakuusikia wameze vizuri mstari hadi mstari halafu mje muwaambie alichopotoshwa Nay ambacho hakijawahi kusemwa na wahanga ni kipi!

=====

Alichojibu Nay wa Mitego baada ya barua hii,

Hii barua ya kufungia wimbo wa 'Nitasema'. Yaani unafungia wimbo ambao mnajua kabisa hakuna media inapiga kwenye nchi hii coz media zote ni chawa wa serikali. BASATA Tanzania haya mąkosa mbona hamkuyaandika kwenye ile hati ya mashtaka mliyonipa?!

Kwaiyo haya ndio mąkosa waliyoyaona na kuufungia wimbo na sijui wanaufungia wapi sasa? Maana hakuna media inapiga nyimbo zangu na nilishasahau mambo ya nyimbo zangu kupigwa radioni sijui kwenye TV!

Kosa la pili mimi mwenyewe ni shahidi nilikosoa kwenye wimbo wangu #wapo nikakamatwa na police na dunia inajua hilo.

Kosa la kwanza tumeona mara kadhaa wanaotekwa na kubahatika kupatikana hai wakisema walio kuja kuwateka walijitambulisha kama police.

Nadhani wote tunajua huu wimbo hauna tatizo ata kidogo na ni wimbo wa kila mtanzania mwenye kupenda amani na upendo viendelee kuta wala nchini kwetu.

PIA SOMA
- Kuelekea 2025 - Haya ndiyo makosa ambayo BASATA wanamtuhumu Nay wa Mitego kutokana na wimbo wake wa Nitasema

- Ney wa Mitego aitwa BASATA kujadili wimbo wake wa ‘Nitasema’
1. Nchi ngapi Afrika ambazo wasanii wanatunga nyimbo na kuimba kwa Kiswahili?
2. Kuna mtu mwenye utambulisho halisi ametajwwa kwenye huo wimbo ambao hauna hata tusi lolote?
3. Tanzania ndio nchi pekee yenye polisi wanaosikika wakitajwa kwenye wimbo wa msanii Ney?
4. Je, utekaji wa aina yoyote haufanyiki Tanzania?
5. Baada ya wimbo huo kusikika kwenye mitandao ya kijamii umesababisha madhara gani na kwa nani na kalalamika kituo gani cha polisi?
6. Mlalamikaji dhidi ya wimbo 'Nitasema' ni nani?
7. Hizo kanuni za BASATA zinazidi sheria?
8. Hisia za BASATA kwamba maadili yamekiukwa zimeanishwa kwenye sheria ipi?
9. Kwanini akina Zuchu waliokuwa wamefungiwa mwaka wamefunguliwa kabla ya muda kuisha kwa kosa ambalo kimsingi ndio lilikuwa kubwa kuweka hisia hadharani za ukosefu wa maadili kwenye maadili kwa vijana na wazazi?
 
Basata ni mzigo mwingine,wanafunga geti wakati farasi Kesha toka.
Kwa teknolojia ya sasa wimbo unasambaa kama moto wa nyikani.
 
Kwamba watu hawajaupata mpaka sasa hivi?🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom