BASATA waufungia wimbo wa Nay 'Nitasema'

Kwani Msomi Mwana FA anasemaje?

Na Ney Wa Mitego angeandika "Njagu" badala ya "polisi" ingeeleweka.

Hivi hawezi kwenda mahakamani?
 
Sawa lakini ujumbe umewafikia na sisi tulisha ipata hiyo nyimbo ipo kwenye simu zetu na PC zetu 😎
 
Sasa wajameni mbona wabongo watu vituko,kwani zile nyimbo chafu chafu za milionea wenu mnayejivunia hamja ziona sembuse kuzisikia?Bongo lala tabu tabu tupu.
 
Hicho ndio kinanishangaza wabongo kweli tumekuwa wajinga wa viwango hivyo?
 
Huyu jamaa anahitaji support sana ya wabongo, nadhani ni msanii pekee ambaye ambaye kwake ishu za Kingono ambazo hata wanyama kama mbwa hufanya, yeye huongelea mambo ambayo ni daraja la la juu la binadam
 
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limeufungia rasmi wimbo 'Nitasema' wa msanii Nay wa Mitego kwa madai ya kukiuka Kanuni ya 25 ya baraza hilo. Katika barua rasmi iliyotolewa na BASATA, wimbo huo umeonekana kuwa na maneno yanayokiuka maadili ya jamii, ikiwemo "wanaokuja kututeka, wanakuja kama polisi" na "na mkikosea, tukikosa, mnatutumia polisi". Maneno haya yametajwa kama yenye ukakasi na kutokuwa na ushahidi wa kuthibitisha madai hayo, hivyo kusababisha kufungiwa kwa wimbo huo kwa mujibu wa kanuni husika.
Nay wa Mitego, kupitia akaunti yake ya Instagram, alijibu hatua hiyo kwa kusema kuwa vyombo vya habari nchini tayari vilikuwa havipigi nyimbo zake kutokana na kile alichokiita kuwa "chawa wa serikali." Nay alieleza kushangazwa na hatua ya kufungia wimbo ambao hata hivyo haukuwa unapigwa kwenye vyombo vya habari.

 
1. Nchi ngapi Afrika ambazo wasanii wanatunga nyimbo na kuimba kwa Kiswahili?
2. Kuna mtu mwenye utambulisho halisi ametajwwa kwenye huo wimbo ambao hauna hata tusi lolote?
3. Tanzania ndio nchi pekee yenye polisi wanaosikika wakitajwa kwenye wimbo wa msanii Ney?
4. Je, utekaji wa aina yoyote haufanyiki Tanzania?
5. Baada ya wimbo huo kusikika kwenye mitandao ya kijamii umesababisha madhara gani na kwa nani na kalalamika kituo gani cha polisi?
6. Mlalamikaji dhidi ya wimbo 'Nitasema' ni nani?
7. Hizo kanuni za BASATA zinazidi sheria?
8. Hisia za BASATA kwamba maadili yamekiukwa zimeanishwa kwenye sheria ipi?
9. Kwanini akina Zuchu waliokuwa wamefungiwa mwaka wamefunguliwa kabla ya muda kuisha kwa kosa ambalo kimsingi ndio lilikuwa kubwa kuweka hisia hadharani za ukosefu wa maadili kwenye maadili kwa vijana na wazazi?
 
..Nadhani wimbo umepigwa marufuku hata hapa JF.
 
Basata ni mzigo mwingine,wanafunga geti wakati farasi Kesha toka.
Kwa teknolojia ya sasa wimbo unasambaa kama moto wa nyikani.
 
Kwamba watu hawajaupata mpaka sasa hivi?🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…