BASATA waufungia wimbo wa Nay 'Nitasema'

Wazee wa Msondo Ngoma nasisi tumehamia kuutafuta huo wimbo, naona hao wanaojiita bakwata sijuhi basata wameupa promotion huu wimbo...mwenye nao anitumie pm huku!
 
Huku TCRA na Jambo TV kule Basata na Ney wa Mitego na bado kuna mpumbafu unaamini Magufuli alipokufa "nchi ikafunguliwa" kama hujuhi neno "system" wewe ni lijinga Sana
 
Wimbo umesambaa kila mahali unaufungiaje?
 
Wazalendo tutausikiliza YouTube. Wafungie na YouTube
 
Ujumbe wa wimbo ulishatufikia watanzania tulio wengi, tutaendelea kuusikiliza
 
Naunga mkonoe hoja kuhusu hiyo message yake ya Instagram
 
Wasanii kibao wameimba nyimbo za kiharakati na kukosoa ila hawajawahi kukamatwa. Mr II, Wagosi wa kaya, Prof Jay na Joh Makini wana nyimbo za kuhoji mambo ya kitaifa lakini hawajawahi kubugudhiwa. Wao hawatumii maneno ya kukera kufikisha ujumbe. Nay wa mitego kwa upumbavu wake hutumia maneno ya hovyo yasiyovumilika ndo maana anasumbuliwa. Wagosi waligusa kila sekta lakini fresh tu walieleweka. Joh Makini baada ya vurugu za Arusha mwaka 2011 alitoa wimbo wa Bye Bye lakini naye hakufanywa kitu. Nay ajifunze kwa waliomtangulia.
 
Wameufungia wakati tunao.

Hao vilaza wa CCM akili hawana.
 
Kwenye globalized world kuufungia wimbo wowote ni kuupa promo.Kila kinachotoka kwenye mtandao kukizuia ni ngumu sana na haiwezekani kamwe
 

..wimbo kufungiwa maana ya ujumbe umefika.

..wimbo wa mwanaharakati usiomkera mtawala haufai.
 
πŸ™‹β€β™‚οΈβœοΈπŸŽ―πŸ‘πŸ‘ŒπŸ‘πŸ‘ŠπŸ€πŸ™πŸŽ–οΈπŸ’πŸŽπŸ†πŸ›‘οΈπŸ‘‘
 
Wazee wa Msondo Ngoma nasisi tumehamia kuutafuta huo wimbo, naona hao wanaojiita bakwata sijuhi basata wameupa promotion huu wimbo...mwenye nao anitumie pm huku!
🀣 🀣 🀣
 
Mkuu tujikite kwenye wimbo huu wa 'Nitasema', ni maneno gani ndani ya wimbo huu ambayo ni ya kukera???

Hebu tuainishie hayo maneno hapa nasi tuyaepuke!! Yanakera kivipi?? Maana hata Basata kwenye hukumu yao hawaja sema yanakera au ni ya hovyo, wamesema wao wameona hayana ushahidi!!

Mkuu wewe hii hukumu yako ya kwamba maneno hayo ni ya hovyo na yanakera umeitoa wapi?? Kwa kanuni na sheria ipi tofauti na ya Basata???
 
Ngoja niutafute huo wimbo nikae pale nikiusikiliza huku nakunywa gahawa

Silence surrenders public responsibilities
 
Nyimbo nyingi za huyu bwana zimejikita kutukana serikali. Sasa najiuliza, watumishi wa serikali(maafisa Utamaduni) ndio wanatoa vibali kwa mtu anayeshambulia na kutukana muajiri wao (Rais)? Hii imekaaje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…