BASATA wawasamehe Diamond na Rayvanny kwa masharti maalumu

BASATA wawasamehe Diamond na Rayvanny kwa masharti maalumu

BASATA wasanii watazidi kuwadharau kwa mtindo huu,adhabu hata haijatumikiwa wameshaiondoa mbona kwenye mpira hatuoni mambo kama hayo!Hao wamesafirije na huku walishanyimwa kufanya show?lazima walijua haiishi siku watasamehewa
 
Barua hii vp
IMG_20181222_124116.jpg
 
Unataka umshauri akiwa anaangalia channel zingine watoto wakalale ?


Huwezi kuangalia baadhi ya vipindi vya TV wakati watoto wako hapo. Watoto wana vipindi vyao maalum, ukibisha aidha huna watoto au TV au vyote.
 
Huwezi kuangalia baadhi ya vipindi vya TV wakati watoto wako hapo. Watotowana vipindi vyao maalum, ukibisha aidha huna watoto au TV au vyote.
Mkuu naelewa
Ila hoja yangu ni kuwa.nyie wenye watoto.uko sebuleni unacheki TV au unachat JF huku TV iko on ghafla upigwe wimbo wowote wa diamond ukabadili chan el ukalutana na mwingine utazima TV ?
Au uko ofisini .huko nyumbani utawaambia wazime TV watoto wakiwa sebuleni ?
 
BASATA wasanii watazidi kuwadharau kwa mtindo huu,adhabu hata haijatumikiwa wameshaiondoa mbona kwenye mpira hatuoni mambo kama hayo!Hao wamesafirije na huku walishanyimwa kufanya show?lazima walijua haiishi siku watasamehewa
unaujua muda usiojulikana???
 
Hilo ni shinikizo kutoka juu... ole wake asipofuata... madhara yake anayajua...


Ataenda kugombaniwa jela...


Cc: mahondaw
 
King Mond watu wenye roho za kimasikini wanakuchukia bure eti wanataka uwalelee watoto
 
Kwa mujibu wa Diamond wakati anaongea na vyombo vya habari nchini Kenya amesema BASATA wamewaruhusu kuendelea na show kwa masharti.

Diamond amesema mara baada ya kupigwa pini ambapo ilikua ni halali kabisa kwa kosa walilolitenda,walichukua hatua ya kuwaandikia barua Baraza hilo la.sanaa kuomba wawasamehe na kuwaruhusu kuendelea na show nyingine jambo ambalo walikubaliwa na kupewa sharti ambalo hakulisema wazi japo aliligusia kwamba wakirudi nyumbani watatakiwa kuteleza.

Mapema leo Wasanii hao ambao wako jijini Nairobi kwa ajili ya show yao ya wasafi festival jijini Mombasa na Nairobi,walionekana kwenye video fupi wakiomba radhi kwa serikali na watanzania kwa ujumla kufuatia kuperform wimbo wa Mwanza uliofungiwa na mamlaka hiyo ya maswala ya Sanaa nchini.

Hata hivyo serikali kupitia BASATA hawajaweka wazi jambo hili la kuwafungulia wasanii hao.
View attachment 973980
Mkuu wamekanusha sasa hatuelewi nani mkweli!
 
Waendelee kupiga kazi kwa nguvu zao zote.....mziki wetu bado una safar ndefu ya kufikia level za kimataifa
 
Back
Top Bottom