Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Uamuzi huo umetolewa baada ya kampuni hiyo kushindwa kutekeleza maagizo halali ya Baraza licha ya kupewa maelekezo kwa nyakati tofauti kupitia barua Kumb. Na. AE/90/90/03/16 ya tarehe 15 Aprili, 2025, na AE.90/90/03/19 ya tarehe 09 Mei, 2025.
Sababu kuu zilizopelekea hatua hiyo ni pamoja na:
1. Kushindwa kuhuisha kibali cha kufanya kazi za sanaa kwa zaidi ya miezi sita bila sababu ya msingi, kinyume na Kanuni ya 39(g) ya Kanuni za BASATA za mwaka 2018.
2. Kukaidi agizo la Baraza kwa kutowasilisha nyaraka muhimu kama nakala ya cheti/leseni ya kushiriki shindano la Dunia, kinyume na Kanuni za 39(f), 37(2)(a) na 36(2).
3. Kushindwa kuandaa shindano la Miss Tanzania kwa mwaka 2023/2024 na kutokuwasilisha mwakilishi wa Tanzania katika mashindano ya Dunia kwa mwaka 2024/2025, bila kutoa sababu za msingi, jambo linalokiuka Kanuni ya 39(i).
Kwa mujibu wa Kanuni ya 40(2) ya Kanuni za BASATA za mwaka 2018, kampuni hiyo imeondolewa sifa ya kuendelea na shughuli hiyo.
Hata hivyo, kampuni ya The Look Company Limited inayo haki ya kukata rufaa kwa Waziri mwenye dhamana ndani ya siku 21 tangu kupokea taarifa hii.
BASATA linaendelea kusimamia kwa ukamilifu utekelezaji wa sheria, kanuni na taratibu katika tasnia ya sanaa ili kulinda heshima na ufanisi wa mashindano ya kitaifa kama Miss Tanzania.
Pia soma ~ Basilla amwambia Rais Samia “Kuvujisha Siri ni utovu mkubwa wa maadili ila kufanya yanayovujishwa ni ukosefu mkubwa zaidi”