BASATA yaufungia wimbo wa Mwanza ulioimbwa na msanii Rayvanny kwa kushirikiana na Diamond Platnumz

Binafsi naona BASATA wamefanya maanmuzi mazuri lakini kwamuda usio sahihi.

Huku ni kutiana hasara tu.
Just imagine msanii ameimba wimbo na ametoa hadi video kwa gharama kubwa ndipo wanafungia wimbo.

USHAURI
Inatakiwa kabla ya msanii kutoa wimbo au nyimbo kwa umma. Nyimbo hizo zikaguliwe ili kuona kama hazivunji tamaduni na kuharibu maadili ya kitanzania.

Basata ipitie nyimbo za diamond zile za nyuma za hivi karibuni nyingi zimejaa lugha ya matusi na hats kama wanatumia tafsida...hizo tafsida ni common sana kufikia kiasi zinaekeweka hata na watoto.

ASANTENI
 
Waufungie na ule wimbo wa kwangwaru...
"Weka mate ili utereze uingie pangoni.." pango gani? utajaza mwenyewe
 
Wamfungie na huyo msanii,ule mdomo mkubwa ameugeuza wa kuimbia matusi badala ya kutumia kula.
 
Huu wimbo unachezwa sana maeneo ya Nyegezi Stand. Na una views 1M sasa hv. Basata wamechelewa.
 
Ndiyo mtakapojua wakisema "huyu hajasoma sana"
 
hata marekani hua kua radio version ya wimbo na explicit version . Wasanii wetu wawe woke
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…