Based on true story: Mahaba yalivyonipeleka kwenye Jamii za Siri Ulimwenguni

Based on true story: Mahaba yalivyonipeleka kwenye Jamii za Siri Ulimwenguni

Tatizo unaleta reference za ulimwengu,
halafu Mimi nakupa facts za kiroho.


siwezi kubishana na binadamu ambaye masaa 24 anashinda duniani, hata kuzimu haufahamu. Wahenga walikwambia, kutembea kwingi ndiyo kuona mengi.
ahsante kwakushiriki chizi maarifa.
Acha vitisho we jamaa hii ni chai kama zilivyo chai nyingne
 
Tatizo unaleta reference za ulimwengu,
halafu Mimi nakupa facts za kiroho.


siwezi kubishana na binadamu ambaye masaa 24 anashinda duniani, hata kuzimu haufahamu. Wahenga walikwambia, kutembea kwingi ndiyo kuona mengi.
ahsante kwakushiriki chizi maarifa.
Endeleza hii kitu!

KULE ushamaliza!!

Nataka nijue hii nini hii!!!
 
Hatutaki CHai hapa. Aende zake huko FB akawadanganye madogo wenzie kisha akawatapeli.
 
Baada ya dakika 15 mkuu wa ukumbi namba 9744, akafika katika jukwaa na wafuasi wake waliketi kimya kwa utulivu wakisubiri kusikiliza neno kutoka kwa mkuu wao.
Wageni wanaruhusiwa kuondoka kabla ya saa 3 usiku ili tubaki na wenyeji, Kuna ibada maalum tutaifanya sisi Wana jumuiya,

Nilikwenda kumuaga yule mwenyeji wangu na kuondoka zangu nyumbani, njiani nilikuwa Nina maswali mengi kuhusu ule mwaliko, hata usingizi sikupata vyema mpaka kesho yake kumekucha. Niliendelea na shughuli zangu za hapa na pale, baada ya siku 3 yule mama Charlotte akanitumia meseji kuwa anaomba mwisho wa mwezi huo tukutane Tena Serena hotel saa 10 jioni, moyoni nilijawa na mashaka, nikajikaza siku ikawadia nikaenda Serena hotel saa 9 jioni nilifika kabla ya saa 10. Nilimuona yule mama Charlotte, akafurahi Sana akaniambia nimepata mwaliko kesho kutwa naomba uvae nguo nyeusi za kupendeza sio Kama ile siku ulivaa kiajabu, hakupendeza, alinipa shilingi laki 480,000/- kwa ajili ya nguo na usafiri hiyo kesho kutwa kuelekea ukumbini 9744.

Saa 12 jioni huu ni muda maalum hutumia kukutana Wana jumuiya wa huu ukumbi namba 9744, nilifika bila kupoteza muda nikajitambulisha kwa niaba ya madam Charlotte, akaambiwa kuwa Kuna mgeni, nikachukuliwa Hadi ndani ya ukumbi 9744, ngoja nikufahamishe jambo, haya majengo hutumiwa kufanya mkusanyiko maalum kwa muda maalum huwa wanaenda na utaratibu maalum hawakurupuki, haya majengo huwa Yana namba zao kutambulisha eneo husika. Kwa nchini Tanzania yapo majengo takribani 7 mkoa tofauti.

Kama kawaida ni mwaliko mzuri wenye kupendeza, watu wa hadhi tofauti na nyadhifa tofauti wakiwa ndani kuendelea na utaratibu, viongozi wa dini, viongozi wa siasa, wasanii, wafanya biashara, Wana michezo, waajiriwa, wakulima, n.k walikuwepo. Ngoja nikufahamishe jambo, ukiwa humu ndani ya jengo, watu wote ni sawa bila kujali umri, kabila, rangi, hadhi yako kimaisha. Hii ni kwa mujibu wa Sheria zao, ikiwa Kuna mwaliko Basi huwa Kuna kutambulishwa wageni wapya, au mshirika wa jumuiya kuapishwa kupanda cheo.

Mkuu wa ukumbi 9744, aliendelea na zoezi la kuapisha na mazungumzo yaliendelea huku akimkaribisha madam Charlotte na wengine kuzungumza chochote kitu katika mwaliko huo. Nilimwona madam Charlotte akisimama na kupongezwa akaanza kutoa hutoba fupi baadae aliniomba kunitambulisha Mimi, nilisimama nikaenda mbele ya jukwaa huku washirika wa ukumbi 9744, wakiwa na nyuso za furaha na uangalizi makini, nilitetemeka nisijue nini hatima yangu mbeleni, madam Charlotte aliniambia kwa upole mwanangu usiogope kuwa jasiri jitambulishe majina yako matatu, umri wako, kazi yako, maono yako mbeleni, bila kupoteza muda nikifanya hivyo nikapongezwa Sana na washirika.
View attachment 2649152
Saa 6 usiku tulimaliza tafrija ile, nikaungana na madam Charlotte kurejea nyumbani, kumbe safari iliendelea mada Charlotte akaomba twende ufukweni, nilihamaki usiku huu tukafanye nini, nimechoka nahitaji kupumzika Sasa, hapana lazima twende mbona kwenye mwaliko umekuja na huku ni lazima ni mwaliko pia, nilishangaa, mwendo wa dakika 35 tufika ufukwe moja wapo jijini dar es salaam, jina nahifadhi, kabla sijashuka kwenye gari lake alinipa maelezo kwa upole, mwanangu unaogopa nini, wenzako wanaitafuta hii bahati wewe unaitupa, hebu kuwa makini na mtulivu Kuna jambo jema kwako mbeleni kuwa msikivu. Nilimsikiliza kwa umakini.

Mwanangu ulishawahi kusikia kuhusu jamii za siri, ndiyo nimewahi kusikia nilimjibu, uliwafahamu vipi..? Aliuliza madam Charlotte. Kupitia mitandao na hadithi za watu nilifahamu Hilo, nilimjibu. Madam Charlotte akatabasamu, akaendelea kuhoji, ulisikia kuhusu nini hizo hadithi. Jamii hizi za Siri wanaua watu, wanatesa, wanakufunga ufahamu nafsi na roho, wanaabudu ibilisi nilimjibu. Dakika hii madam Charlotte akacheka kwa nguvu, akasema hao ni waongo hebu ushuhudie mwenyewe kwa macho. Nishuhudie vipi..? Nilihoji. Usiwe na shaka mwanangu Mimi nipo ngazi ya juu, mkuu wa ukumbi namba 84 nchini uingereza. Katika washirika wa kike tu bila wanaume. Hivyo nimekuleta hapa ufanye jambo moja tu. Umeona ile gari pale ni gari ilikuwa mbele yetu ufukweni Aina ya Land cruiser v8, nyeusi. Akanipa kadi yake akanipa na kutambulisha nivae, nikapewa maelezo,

Taratibu nilishuka garini, nikaelekea kuifuata ile gari nyeusi, niligonga kioo Cha gari nikafunguliwa mlango nikaingia ndani, nilimwona kijana ambaye ni mwasiasa, ni mbunge wa Jimbo fulani, kwa heshima na kanuni, Sheria za kifungu katika mwongozo wa jumuiya ya jamii hii ya Siri nitahifadhi jina lake. Nilishangaa kumwona akanikaribisha nilimwonyesha kadi yenye taarifa za madam Charlotte, na kitambulisho changu Kama ishara fulani, tuliongea mengi kwa muda wa saa 2 nzima, alinieleza kuhusu faida za kikundi Chao, asili yao, na utaratibu wao, tulizungumza mengi, baada ya masaa 2, nilirudi kwa madam Charlotte na kumweleza niliyo kwisha kuelezwa, alifurahi Sana akaniambia si muda mrefu utapata mwelekeo bora, mwangaza bora, utu bora, thamani bora, heshima tukufu ikiwa utaungana nasi, tulirudi majumbani kwetu nikiwa nimechoka mno hasa kwa mawazo. Siku 30 zilipita sawa na mwezi mmoja, japo kuwa niliendelea kuwasiliana nao huku wanipa morali, usawa, na matumaini. Katika moja wapo ya majira nilipata ujumbe kutoka kwa madam Charlotte kuwa nijiandae Kuna mwaliko wa muhimu na itapendeza niwepo pale ukumbi wa 9744.

MKASA HUU UTAENDELEA, TUONE HUO MWALIKO MUHIMU ILIKUWAJE....?
Bwana Lucifer hii story imekushinda tuombe msamaha wana JF
 
Back
Top Bottom