saidoo25
JF-Expert Member
- Jul 4, 2022
- 624
- 1,456
Waziri Bashe jioni hii akichangia bungeni ameutupia lawama Mhimili wa Bunge kuwa ndio umesababisha kuharibu kilimo na kusisitiza kuwa kamwe Serikali ya Rais Samia haiwezi kufanya kosa hilo.
Pamoja na lawama hizo nzito kwa watunga sheria..Kiti hakijaweza kutoa mwongozo wowote kuhusiana na jambo hili la Waziri kulidharau Bunge, wakati Rais mwenyewe wa nchi Dk. Samia Suluhu Hassan hajawahi kulidharau Bunge wala wabunge kwa kuwa anatambua ni moja ya mihimili ya nchi iliyoko kwa mujibu wa Katiba.
Swali la muhimu. Bashe anapata wapi kiburi cha kulidharau bunge kwa kiwango hicho ilihali Rais Samia mwenyewe anayemwakilisha kwenye wizara ya kilimo hajawahi kutoa kashfa kwa Bunge, ametumia bunge kuwatetea wafanyabishara na kusisitiza kuwa kamwe serikali haiwezi kuwapangia bei ya kuuza mazao yao.
Je Wabunge nao wakiamua kueleza ukweli juu ya makampuni yanayohusika na kuuza mazao ndani na nje ya nchi na mahusiano yao na Bashe yuko tayari kuwajibika?