Bashe hadi sasa bado ni Waziri wa Kilimo? maajabu ya dunia

Bashe hadi sasa bado ni Waziri wa Kilimo? maajabu ya dunia

Stuka

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2022
Posts
282
Reaction score
906
Tumemsikia Mpina kashfa ya kuagiza sukari kutoka nje, tumewasikia wakulima wa miwa wakimlalamikia Bashe kwa kuua kilimo chao cha miwa, tumewasikiliza wenye viwanda wakimlalamikia bashe kwa kutunga sheria ya kuua viwanda vyao, tumemsikia Mheshimiwa Rais akilalamikia suala la uagizaji sukari nje ya nchi kwamba viwanda vyetu vinajitosheleza kuzalisha sukari..

Bado wakulima wa tumbaku wanamlalakia, wakulima wa mpunga wanamlalamikia, wakulima wa mkonge wanamlalamikia, wakulima wa chai wanamlalamikia, wakulima wa mahindi wanamlalamikia, lakini bado hadi leo anasifa za kuendelea kuwa waziri wa kilimo ni ajabu na kweli.

Hao wote wameonyesha Bashe amepoteza sifa za kuwa waziri wa kilimo lakini nashangaa hadi sasa bado anasimama kwenye ziara ya rais na kuendelea kumpa matakwimu yake ya uongo kuhusu kilimo
 
Kwenye sugar wamekula wootee na yuleeeeee pia amekulaaamooo
 
Back
Top Bottom