Bashe yupo ukingoni, hakupaswa kupambana na wadau wa sukari

Bashe yupo ukingoni, hakupaswa kupambana na wadau wa sukari

August 83

Member
Joined
Apr 8, 2024
Posts
29
Reaction score
61
Bashe ambaye ni Mbunge wa Nzega mjini na Waziri wa Kilimo wa Serikali ya Rais Samia dalili zi wazi anaelekea kukwama.

Kwa wajuzi wa mambo ya siasa watakubaliana na mimi kwenye hilo.

Waziri Bashe hakupaswa kupambana na wadau wa sukari kwa aina ile ya kiburi na majivuno! Kwa kuanzia alipaswa kubadili sheria ya uagizwaji sukari nje na siyo kubadiri kanuni pekee.

Pona yake labda ahamishwe Wizara. Tofauti na hivyo wenye sukari yao watamng'oa pale kwa gharama yeyote!

Mpina ndiye atakuwa mwiba mkali utakao endelea kutumiwa kupewa nyaraka muhimu za kummaliza.

Tatizo Bashe na Mwigulu wanataka kupambana na Mpina bila akili huku wakisahau huyo huyo Mpina anaweza kuwa anapewa information zao muhimu za kuwamaliza.

Samia ili kumnyamazisha Mpina labda amteue awe Waziri. Vinginevyo, Mpina ataiangusha Serikali yake mle Bungeni.

Pia soma:
- Kama kweli Waziri Bashe katoa kibali cha kuagiza Sukari kwa kampuni ya simu, hii haitakuwa na tofauti na Ufisadi wa Lowassa Richmond

- Luhaga Mpina amshukia Waziri Bashe, adai amelidanganya Bunge, awataja Magufuli, Rais Samia
 
Jamaa bado yupo sana labda kama Mpina angekuwa na lakukumbukwa nchi hii!.
 
Na amini wewe ni mwanaume,usitumie hisia kufikiri be a critical thinker
Hifadhi hilo nililokujuza na kwa mapenzi ya Mungu rejea tena mwezi wa 6/ 2025 baada ya Mkutano mkuu wa CCM wa kumteua mgombea wa u Rais kupitia chama chao.
 
Bashe hawezi kung'olewa, kwani kwa kufanya hivyo atainajisi serikali yake. Ukizingatia tunaelekea kwenye uchaguzi.
 
Bashe ambaye ni Mbunge wa Nzega mjini na Waziri wa Kilimo wa Serikali ya Rais Samia dalili zi wazi anaelekea kukwama.

Kwa wajuzi wa mambo ya siasa watakubaliana na mimi kwenye hilo.

Waziri Bashe hakupaswa kupambana na wadau wa sukari kwa aina ile ya kiburi na majivuno! Kwa kuanzia alipaswa kubadili sheria ya uagizwaji sukari nje na siyo kubadiri kanuni pekee.

Pona yake labda ahamishwe Wizara. Tofauti na hivyo wenye sukari yao watamng'oa pale kwa gharama yeyote!

Mpina ndiye atakuwa mwiba mkali utakao endelea kutumiwa kupewa nyaraka muhimu za kummaliza.

Tatizo Bashe na Mwigulu wanataka kupambana na Mpina bila akili huku wakisahau huyo huyo Mpina anaweza kuwa anapewa information zao muhimu za kuwamaliza.

Samia ili kumnyamazisha Mpina labda amteue awe Waziri. Vinginevyo, Mpina ataiangusha Serikali yake mle Bungeni.
Dogo inawezekana hukusilikiza Hotuba ya Bajeti ya Mwaka 2024/2025. Kama ungeisikiliza usingeandika haya.
 
"Wenzetu" wanajadili AI sisi tunajadili sukari! Kweli!
Tutafanyaje sasa mkuu na asubuhi tunataka chai yenye sukari na vitumbua vyenye sukari. Ubongo ukikosa sukari ya kutosha hata hiyo AI haifikiriki achilia mbali kuijadili
 
Habari wakuu!

Baada ya kumsikiliza mpina kwa umakini nilitegemea lucas mwashambwa muimba mapambio kindaki ndaki na mzalendo wa CCM angejitokeza kumsihi waziri bashe kuachia ngazi! Ila nashangaa kimya swali kwako Lucas Mwashambwa.

1: Umekubaliana na mheshimiwa mpina umeamua kumuachia speaker?
2: Wewe ni mzalendo kwa wala rushwa na wezi?
3: Kwa kuwa wewe ni ccm unayesifia kila kitu huruhusiwi kukosoa pia?
4: Ukiwa ccm unasupport kila kitu hata uozo?
5: Je, upo kusifia kutafuta teuzi au upo humu kama chawa wa CCM
6: Una maoni gani juu ya hili?
7: Ni kweli kwamba lucas mwashambwa Elimu yako imeishia kusifia tu?? Lakini sio kukosoa na kukemea
 
Dah jamaa atakua na machozi mengi sana mana kila siku anabubujikwa na machozi ya furaha kuhusu ccm.
 
Back
Top Bottom