Hatua ya kuacha kulalamika tu na kuingia mahakamani kutafuta haki, ni hatua ya muhimu sana katika maendeleo.
Ni hatua ambayo inaweza kumtoa unyonge mtu, mtu ambaye haki anaweza kuwa nayo, tatizo ikawa ni kujipanga kuidai tu.
Hatua hii pia inasaidia kufungua macho wengine, nao wasema "aah, kumbe hili linawezekana".
Zaidi, ni hatua itakayoweka historia ya kisheria (legal precedent) kiasi kwamba wafanyabiashara wengine wote wa hii biashara, kama mahakama itaamua kukubaliana na madai ya mfungua kesi, itawabidi wabadikishe mienendo yao ama kuwa katika fungu la kuvunja sheria.
Historia hii ya kisheria itasaidia hata mbele makampuni mapya yakianzishwa, au vifurushi vipya vikianzishwa na kampuni za sasa, kampuni zitatakiwa kuzingatia maamuzi ya mahakama.
Tunahitaji utamaduni wa kushitaki mahakamani kudai haki, na kuacha kulalamika tu, si katika hili tu, bali katika mengine mengi sana.