Bashir Yakub: Nitayashitaki makampuni manne ya simu

Bashir Yakub: Nitayashitaki makampuni manne ya simu

Ni ukweli wanatuibia. Tena sana. Ila kwa hizo pesa wanazotuibia they'll pay an army of lawyers na kama una nguvu ya kutosha labda unaweza ukawakimbiza. Kama una nguvu
 
Hahaaa mkuu naomba uniunganishe kwenye hii kesi,juzi nimeishia kucheka badala ya kulia!! Ni hivi,nimenunua kifurushi cha Gb moja kutoka HALOTEL kwa njia ya haloPesa,nikawasha data na kuanza kupepesa macho kwenye mitandao hasa hapa Jf,sija stream video hata moja,baada ya kama lisaa limoja nikapata meseji, "umebakiwa na mb 5 tu.

tafadhali bonyeza *148*66# kupata kifurushi kingine" nikaamua kuzima data kabisa muda huo huo na kununua kifurushi kingine kwa mtandao tofauti,nikapata gb moja(ndiyo hii nnayoitumia hadi sasa) basi nikawasha tena data na kuendelea kuperuzi kwa hiki kifurushi kipya,baada ya dakika mbili tena nikapata massage!! Inatoka halotel! ! "Kifurushi chako cha wiki kimeisha,tafadhali bonyeza *148*66# kupata kifurushi kingine" !!!! Nikajiuliza hawa halotel nimewakosea nini? Nikajokuta tu nacheka,yaani natumia airtel lakini bando la halotel ndiyo linakwisha? Nimewavulia kofia.
 
Hapo namba 3 upande wa MB ndo khatari tena zaid ya sana. Unakuta umejiunga GB zako then kitendo cha kuwasha Data On na kuperuzi page kadhaa basi washalamba MB kadhaa yam jamaa ni noumer nipo pa1 nawewe mtoa mada[emoji106][emoji106][emoji106]
 
Wazo zuri, na umedadavua haswa japo watakwambia wameweka kifurushi cha bila ukomo. Kwa jicho la kiuchumi kwao watashuka kimapato, kinyume chake itakuwa nafuu kwa mteja.
 
Capt Tamar, Mkuu serious?[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16] mimi nauhakika hivi vifurushi huwa hawatupi vyote kama wanavyoandika ktk menu zao, niliwahi kujiunga na kifurushi cha Voda internet cha GB 1 niliingia jf kama dk 15,fb kama dk 10,huko YouTube niliingia kucheki video ya dk 4 tu,hapohapo nikaambiwa nimebakiwa na mb 12
 
Hatua ya kuacha kulalamika tu na kuingia mahakamani kutafuta haki, ni hatua ya muhimu sana katika maendeleo.

Ni hatua ambayo inaweza kumtoa unyonge mtu, mtu ambaye haki anaweza kuwa nayo, tatizo ikawa ni kujipanga kuidai tu.

Hatua hii pia inasaidia kufungua macho wengine, nao wasema "aah, kumbe hili linawezekana".

Zaidi, ni hatua itakayoweka historia ya kisheria (legal precedent) kiasi kwamba wafanyabiashara wengine wote wa hii biashara, kama mahakama itaamua kukubaliana na madai ya mfungua kesi, itawabidi wabadikishe mienendo yao ama kuwa katika fungu la kuvunja sheria.

Historia hii ya kisheria itasaidia hata mbele makampuni mapya yakianzishwa, au vifurushi vipya vikianzishwa na kampuni za sasa, kampuni zitatakiwa kuzingatia maamuzi ya mahakama.

Tunahitaji utamaduni wa kushitaki mahakamani kudai haki, na kuacha kulalamika tu, si katika hili tu, bali katika mengine mengi sana.
 
Andiko zuri sana. Na katika sector ambayo inadhulum Wananchi sana na hizi za mawasiliano. Pesa hukatwa kienyeji saana. Mambo za vifurush na huduma mbovu.

Ila deal na kipengele cha sheria vizuri. Huwa wameweka option ya kukubali au kukataa wakiwa na maana ukikubali basi vigezo na taratibu zote umekubaliana navyo. Na ukikataa pia huwa ni sawa kwako.

Kitengeneze hiki vizuri tukaliamsha
 
Back
Top Bottom