Bashir Yakub: Nitayashitaki makampuni manne ya simu

Bashir Yakub: Nitayashitaki makampuni manne ya simu

Mkuu kwani unaponunua bidhaa dukani ukaitumia nusu na nyingine ikabaki, ukafika muda wa ku expire utaenda kuuliza kwa nini ime expire kabla ya kwisha?! Makubaliano ni hayo ya kwenye kifurushi, masaa au siku au mwezi. Kama hutai jiunge na huduma ya malipo baada ya matumizi kwnye hiyo mitandao.
utakuwa umeajiriwa na haya makampuni.

hivi unapataje ujasiri wa kupinga kilio cha wengi?
 
Tanzania inaongoza kwa kutoza viwango vikubwa vya intaneti katika nchi za Afrika Mashariki.
Kwa mujibu wa cable.co.uk,Zimbabwe inangoza duniani kwa na gharama za intaneti ambapo gigabaiti 1(1GB) inagharimu dola za kimarekani 75.2 (TZS.172,847),ikifuatiwa na Equatorial Guinea dola za kimarekani 65.83.
India inaongoza kwa kuwa na kiwango kidogo ambapo1GB ni dola za kimarekani 0.26 (TZS.598).
Huku Tanzania ikiongoza kwa gharama kubwa Afrika Mashariki na Kati.View attachment 1253780
Kwa takwimu hizo ulizoonyesha hapo, ni kweli gharama ya kutumia intaneti ziko juu Tanzania ukilinganisha na nchi za Afrika Mashariki. Hiyo inatokana na idadi ya watumiaji, ni simple economics, kuwa watumiaji wa bidhaa fulani mkiwa wachache, yule mwenye kuuza hiyo bidhaa atawatoza zaidi ili kufikia gharama zake za uendeshaji na apate faida pia.

Sababu nyingine ni ukosefu wa ushindani makini katika soko la Tanzania la intaneti, akipata anaye toza chini ya hii ya sasa na hivyo kuleta ushindani sokoni, hao wengine watashusha pia gharrama zao. Hivyo tuwaombe TTCL wakaze buti wayashinde haya mengine na AIRTEL ambao ni ya kwetu nao waambiwe wapunguze gharama zao. N a zaidi, ni vizuri watumiaji wa Intaneti muongezeka ili watoa huduma hizi washushe bei zao, AU SIYO?
 
utakuwa umeajiriwa na haya makampuni.

hivi unapataje ujasiri wa kupinga kilio cha wengi?
Hujanijibu swali umeendeleza vioja, kilio kiwe cha utaratibu wa kujiunga na vifurushi visiwe na mwisho wa matumizi bali umalize hela yako.
 
Hujanijibu swali umeendeleza vioja, kilio kiwe cha utaratibu wa kujiunga na vifurushi visiwe na mwisho wa matumizi bali umalize hela yako.
Masharti unayoyazungumza hapa yalifanyika kwa makubaliano kati ya mtandao na mteja au kwa lazima kwa mtandao kujiamulia utakavyo na kuyaita masharti na vigezo? Unapopewa masharti yenye unyang'anyi na ukandamizaji bado unafikiri yanastahili kuwa na hadhi ya masharti? Unanunua line ya Simu leo, kesho wanaamua tu kubandika masharti yao, wewe haki yako inakuwa ni kukaa kimya kisa tu masharti na vigezo kuzingatiwa? Hayo masharti huwa tunapewa wakati wa kununua hizo simu kwamba tunakubaliana nayo au yanatukutia juu kwa juu baada ya kuanza kutumia simu?
 
Mkuu kwani unaponunua bidhaa dukani ukaitumia nusu na nyingine ikabaki, ukafika muda wa ku expire utaenda kuuliza kwa nini ime expire kabla ya kwisha?! Makubaliano ni hayo ya kwenye kifurushi, masaa au siku au mwezi. Kama hutai jiunge na huduma ya malipo baada ya matumizi kwnye hiyo mitandao.
Japo mfano wako hauendani sana kutokana na utofauti wa bidhaa, bidhaa ya dukani ikieksipaya, mwenye duka anakuja kuichukua au unabaki nayo uamue mwenyewe nini utafanya?

Magari mangapi yanatembelea matairi yaliyoeksipaya? Si ni kufanya mammbo at your own risk..kama mitandao inaona lazima kuwe na expiry, basi wasichukue data zilizochacha waziache tu uziangalie mwenyewe uliyezinunua..wanaweza kutokea watu wengine wakawa wananunua data chakavu
 
naona una uswahiba na hii mitandao kama bado unaona kilio chetu kama kioja na ukamuaji wa jasho la watanzania bila watetezi.

kuitwa 'makubaliano' ilipaswa kampuni ijadili na mlaji kabla ya kuanza mchakato wa utekelzaji. lkn kwasasa unaamka na kukuta mabadiliko tu na hakuna mjadala unaanza kufuata bila mjadala, iweje wewe uyaite makubaliano?

kifurushi hakitakiwi kuwa na mwisho wa matumizi madhari umeshakilipia, sio tupangiwe lini tutumie.
Hujanijibu swali umeendeleza vioja, kilio kiwe cha utaratibu wa kujiunga na vifurushi visiwe na mwisho wa matumizi bali umalize hela yako.
 
Kila kheli make tunanyanyasika kwelikweli Mungu atakuwa juu yako kwa kutetea watanzania wanyonge hawa hasa wa vijijin ambapo umeme ni shida ama mtandao shida
 
Hivi hizi msg hazihitaji kuwe na subscription? Au ndio terms and conditions zao sikuzisoma wakati nanunua line ya Vodacom.
54E81740-A1C4-47AA-BF96-5D4261F76351.png
 
albertdaniel, Mkuu acha kuita OFFER
Hizo ndizo product wanazotuuzia ila wao wanaita OFFER ili kutuhadaa
 
Sina haja ya salamu, nimekereka haswaa.

Haya makampuni ya simu yalishageuza nchi hii kama shamba la bibi, wanavuna watakavyo. Gharama za kutoa pesa kwa njia ya mtandao zimeongezeka mara dufu.

Achana na hiyo, kuna gharama za vifurushi na data huko ni hatari. Hao Vodacom ni kama data huwa tunatumia pamoja maana wanakula data mpaka unashangaa kwamba ni wewe umetumia data peke yako au kuna mtu mwingine mnasaidiana.

Hivi nchi hii kuna watu wanaojali hali ya maisha ya mtanzania wa chini?.

Hebu angalia Vodacom hawa vifurushi vyao vya wiki. Na hii siyo Vodacom pekee bali ni mitandao yote yani wanatatafuna nchi hii bila huruma
IMG_20191209_064529_806.JPG
 
Mtafunaji wa kwanza ni huyo unayepeleka malalamiko. Anawatafuna kwa mabilioni ya faini kisha anakusanya na kuweka kodi mpya kama kawaida
 
Kinachonishangaza zaidi ni wewe hapo kuwang'ang'ania Voda wakati hawakutaki, ,Akufukuzae hakwambii Toka,
SI UHAME KWANI MTANDAO NI MMOJA?

Kila siku mnalia lia huko mtafikili mmefunga ndoa ya kikiristu na VODA;

Kama ni ndoa basi ficheni siri ya kitanda, mbona mkipata utamu hamsemi? lakini Mme akichepuka mnalalama?
Mkipewa GAWIWO mnakenua lakini mkikatwa mnalia!
HAMENI BHANA MSITUCHOSHE
 
Bado hujaijua internet ya voda ilivyo na kasi, bado hujajua walivyo very fast kusaidia wateja wao.
Wako vizuri sana tatizo lako gharama kubwa mno
 
Back
Top Bottom