Uchaguzi 2020 Bashiru: Kuna mtu unakuta ndani ya miaka mitano tu kapata vyeo vikubwa viwili kwa mpigo halafu kabla hajakomaa pale, anataka Ubunge. Sigombei

Uchaguzi 2020 Bashiru: Kuna mtu unakuta ndani ya miaka mitano tu kapata vyeo vikubwa viwili kwa mpigo halafu kabla hajakomaa pale, anataka Ubunge. Sigombei

Yeye mwenyewe kapanda sana ngazi pasipo kupita madaraja.
Kutoka kusikojulikana hata hatujasikia akiwa mwenyekiti wa shina mpaka kuwa Katibu mkuu !!!
Atulie tu

Sent from my A50s using JamiiForums mobile app
 
Nikikuambia kuwa ccm wanatumia mabavu ya vyombo vya dola kuongoza kwa shuruti, sina chembe ya shaka na maelezo yangu. Kutekeleza mipango ya maendeleo ya vitu au watu, ni wajibu wa serikali yoyote, hata wakoloni walifanya hilo. Kwamba vyombo vya dola vimetumika kukandamiza upinzani, hilo halihitaji hata kuishi hapa nchini kujua hayo.

Kama mnaamini ni wajibu wa Serikali kutekeleza mipango ya maendeleo na ikatimiza wajibu huo, kuna hoja gani tena ya msingi?

Kwa nchi zinazoendelea kumekuwa na mapungufu makubwa ya kiuongozi, hasa kuhusu matumizi ya kodi na usimamizi wa rasimali za Taifa. Uongozi wa Magufuli umethibitisha kuwa ni imara katika matumizi na usimamiaji, na ndiyo maana sina shaka kuwa Serikali ya CCM itarudishwa madarakani.

Kwamba hata wakoloni walifanya hivyo, ni hoja ya kipuuzi, kwani ukoloni ulifanya hivyo kurahihisha utawala wao tofauti na ilivyo sasa. Mahitaji na mipango ya maendeleo hutoka kwa wananchi kupitia wawakilishi wao toka ngazi za chini. Wananchi waliochagua wawakilishi makini na waadilifu, hakuna shaka maeneo yao yana maendeleo yanayoonekana.

Nisingependa kutoa mifano jinsi vyama vya upinzani vinavyotumia ruzuku (kodi ya wapiga kura) kunufaisha wanasiasa viongozi wa vyama hivyo huku wakitegemea kesho wapewa dhamana ya kuongoza nchi.

Au mnadhani wapiga kura ni wajinga kiasi cha kutokutambua mbivu na mbichi? Labda mnaamini Tume Huru ya Uchaguzi ndiyo agenda ya kuaminisha wapiga kura?
 
Bashiru acha kuwapangia watu. Mwacheni Bashite atimize ndoto zake. Na mkimkata atakwenda kwa baba yake mzee Membe. Kigamboni pale lazima ashinde uchaguzi mkuu.
 
Bashiru acha kuwapangia watu. Mwacheni Bashite atimize ndoto zake. Na mkimkata atakwenda kwa baba yake mzee Membe. Kigamboni pale lazima ashinde uchaguzi mkuu.

Rukhsa kuhama ili atimize ndoto yake kwani wanaohama vyama vya siasa ni wengi tu. Ila CCM ina itikadi yake ya kulea viongozi wenye mtazamo wa kitaifa na si wa kutimiza ndoto zao.

Labda kama ulikuwa hujui, ukidhani ni
Bashiru, Katibu Mkuu, ndiye kikwazo, sifa za kiongozi CCM ziko kwenye Katiba ya Chama (1977):
17. Pamoja na kutimiza masharti ya Uanachama kama yalivyoelezwa katika Katiba, Kiongozi sharti pia awe na sifa zifuatazo:-
(1) Awe ni mtu aliyetosheka na asiwe mtu aliyetawaliwa na tamaa.
(2) Awe ni mtu anayependa kueneza
matunda ya Uhuru kwa wananchi wote kwa ajili ya manufaa yao na maendeleo ya Taifa kwa jumla.
(3) Awe na sifa nyingine kama zilivyowekwa katika Kanuni zinazohusika.
 
Bashite ni exceptional. Kama hawamjui Mwenyekiti wa watafurahi wenyewe
 
Kuoneana tu, kwani ubunge ni CHEO cha utumishi wa umma hadi kihitaji experience ya miaka kadhaa? Mbona kina Mkosamali walitoka shule hadi bungeni au kina Musukuma walikuwa ma RC wapi? Hoja za wasomi wa nchi hii bwana.
 
Nikikuambia kuwa ccm wanatumia mabavu ya vyombo vya dola kuongoza kwa shuruti, sina chembe ya shaka na maelezo yangu. Kutekeleza mipango ya maendeleo ya vitu au watu, ni wajibu wa serikali yoyote, hata wakoloni walifanya hilo. Kwamba vyombo vya dola vimetumika kukandamiza upinzani, hilo halihitaji hata kuishi hapa nchini kujua hayo.
Kwani ni lazima afanye kazi mliyoamua nyinyi. Wapeni haki ya kuchagua. Hoja mnazotoa ni manyanyaso kwao.
 
Mwambieni Bashiru kuwa ubunge una posho nzuri na pensheni yake ni ya kutosha tu
 
We
Kama mnaamini ni wajibu wa Serikali kutekeleza mipango ya maendeleo na ikatimiza wajibu huo, kuna hoja gani tena ya msingi?

Kwa nchi zinazoendelea kumekuwa na mapungufu makubwa ya kiuongozi, hasa kuhusu matumizi ya kodi na usimamizi wa rasimali za Taifa. Uongozi wa Magufuli umethibitisha kuwa ni imara katika matumizi na usimamiaji, na ndiyo maana sina shaka kuwa Serikali ya CCM itarudishwa madarakani.

Kwamba hata wakoloni walifanya hivyo, ni hoja ya kipuuzi, kwani ukoloni ulifanya hivyo kurahihisha utawala wao tofauti na ilivyo sasa. Mahitaji na mipango ya maendeleo hutoka kwa wananchi kupitia wawakilishi wao toka ngazi za chini. Wananchi waliochagua wawakilishi makini na waadilifu, hakuna shaka maeneo yao yana maendeleo yanayoonekana.

Nisingependa kutoa mifano jinsi vyama vya upinzani vinavyotumia ruzuku (kodi ya wapiga kura) kunufaisha wanasiasa viongozi wa vyama hivyo huku wakitegemea kesho wapewa dhamana ya kuongoza nchi.

Au mnadhani wapiga kura ni wajinga kiasi cha kutokutambua mbivu na mbichi? Labda mnaamini Tume Huru ya Uchaguzi ndiyo agenda ya kuaminisha wapiga kura?

Mwengeso unajua unachoongea? Kutekeleza mambo ya maendeleo ni wajibu wa serikali. Inaonekana unachanganya kati ya chama na serikali. Serikali huwa ipo tu hata kama aliye madarakani kaingia kwa kupindua nchi. Serikali inaweza kuongozwa na chama chochote. Huenda ww ni mzee, ambaye hajawahi kuona serikali ikiongozwa na chama kingine, hivyo unadhani ccm ndio serikali. Hii ndio imepelekea ww kuongea ulichoongea paragraph ya Kwanza.

Ni kweli ccm inaweza kurudishwa madarakani kuongoza serikali, lakini mazingira yaliyopo ndio yanaifanya ccm kurudi madarakani, sio kwa kukubalika zaidi, bali uwepo wa tume isiyo huru ya uchaguzi, na matumizi ya vyombo vya dola, huku taasisi nyingine za kimamlaka kudhani wao wana wajibu wa kuifanya ccm ikae madarakani. Hivyo ccm iko madarakani kwa shuruti zaidi kuliko kupitia ridhaa ya wananchi.

Unaandika maneno mengi, lakini mtu akifuatilia vizuri unachoongea ataona fika ulivyo na uelewa finyu wa mambo. Sasa kama hujui tofauti ya chama na serikali, huoni lazima utajikuta unaongea maneno mengi yasiyo na maana yoyote?

Kwa taarifa yako wakati wa uchaguzi kinachoshindanishwa ni ilani, ni kweli chama kilichoko madarakani kina faida fulani ya kusema kuwa kimefanya nini,lakini washindani wake wanaweza kuja na ilani bora, ambayo wanaweza kupewa ridhaa na wananchi ili waongoze serikali. Hapa ndio maana tunataka tume huru ya uchaguzi,kwani kuwa tume iliyopo inachaguliwa na mwenyekiti wa ccm, hivyo inadhani ina wajibu wa kumtangaza mwenyekiti wa ccm, na chama chake kuwa ndio washindi. Na kwa ajili ya muundo huu usiokubalika wa tume, rais anaweza kuipa amri atakavyo kwa kudhani yeye ndio msimamizi wa hiyo tume, hivyo ni lazima itii atakacho kwani yeye ndio anawalipa.
 
We

Serikali inaweza kuongozwa na chama chochote.

Unaandika maneno mengi, lakini mtu akifuatilia vizuri unachoongea ataona fika ulivyo na uelewa finyu wa mambo. Sasa kama hujui tofauti ya chama na serikali, huoni lazima utajikuta unaongea maneno mengi yasiyo na maana yoyote?

.

Kama ni kujichanganya ni wewe. Nimeacha aya hizo mbili ulizoandika wewe.

Kwa Katiba ya JMT, hakuna mgombea binafsi hivyo mgombea wa Urais ndiye uunda Serikali. Na mgombea Urais huteuliwa na chama na kunadi Sera za chama kama zilivyoanishwa kwenye Ilani.

Awali nilisema Serikali imetekeleza yaliyomo kwenye Ilani kwa sababu ya usimamizi makini wa Chama. Hivyo chama, kwa maana ya wagombea, watapanda kwenye majukwaa ya kampeni wakiwa wamebeba mafanikio yaliyotokana na utekelezaji wa Ilani yake na Serikali.

Je, upinzani unalo lipi la kunadi iwapo katika kipindi chote ni kuibeza Serikali pasipokuwa na Sera mbadala! Upinzani ukipanda majukwaani kudai Tume Huru au demokrasia, wataeleweka?
 
Hayo ndio matamanio yako kuwa upinzani usiwe na cha kueleweka. Ww na serikali ya ccm mnadhani ndio mnaeleweka mkisema hamtaki tume huruma na demokrasia? Sera mbadala ni hizo wanazotaka ccm? Subiri wakati wa kampeni utasikia, labda tume hii iendelee kuibeba ccm.

Hata hivyo sera za ccm ni zipi? Maana huwa nasikia mkisema mleta barabara, maji, umeme, reli nk. Je kikiingia chama kingine hakitaleta hiyo miundombinu, je hiyo miundombinu ndio sera? Maana hata serikali ikiingia kwa kupindua bado itafanya hivyo hivyo vitu, je hiyo miundombinu ndio sera?
 
Duniaaa, haina huruma eeeh! ×2

Nimejikuta namuimbia Nape kawimbo.
Anapitia kipindi kigumu sana awamu hii. Mara anyooshewe mguu wa kuku hadharani, hatujakaa sawa anapiga magoti kuomba radhi, na Sasa anajificha hata kuchukua fomu.

Nape, ooooh Nape!
😃😃😃😃 daah we jamaa umenchekesh kwel nape wa 2010-2015 cio huyu wa sasa kabsa kawa mnyonge hata kuongea hawezi daah magu co mtu mzur kwa kwel
 
Hahahaha aibu kubwa sana hii. Wanamuogopa Makonda utadhani ukoma dadeeeki
Wew humwogopi? Hizo siri zote alizonazo kuhusu zile maiti zilizokuwa zinaelea baharini ni kitu kidogo? Kujua Ben Saanane alienda wapi ni kitu kidogo?. Ni Pompeo tu ndo hamwogopi Bashite maana aliweka wazi kuwa "ananyima watu haki ya kuishi"
 
😃😃😃😃 daah we jamaa umenchekesh kwel nape wa 2010-2015 cio huyu wa sasa kabsa kawa mnyonge hata kuongea hawezi daah magu co mtu mzur kwa kwel
Kwakweli Magu amefifisha nyota na kuzima ndoto za Nape
 
Wew humwogopi? Hizo siri zote alizonazo kuhusu zile maiti zilizokuwa zinaelea baharini ni kitu kidogo? Kujua Ben Saanane alienda wapi ni kitu kidogo?. Ni Pompeo tu ndo hamwogopi Bashite maana aliweka wazi kuwa "ananyima watu haki ya kuishi"
Dah Usiku mwema
 
Kuhusu kutenda haki kwa wagombea wote, Dkt. Bashiru amesema:

”Nadhani kama umemsikiliza Mwenyekiti wetu jana wakati anaapisha baadhi ya viongozi, alisema yeye kama mwenyekiti wa chama hana mgombea, na akaenda mbali kusema Makamu wa Rais, hana mgomnea; akamtaja Waziri Mkuu, hana mgombea; akamtaja Makamu Mwenyekiti, Mzee Mangula, hana mgombea; akanitaja mimi, sina mgombea.”

“Matarajio yetu, viongozi wanaokaa kwenye vikao vya uteuzi wana dhamana kubwa ya kutenda haki kwa wagombea wote. Hata kama ni mkeo, hata kama ni mwanao, hata kama ni rafiki yako mulisoma wote, hata kanma ni tajiri yako kakuajiri – unalinda maslahi ya chama siyo maslahi ya mgombea. Na kwahiyo upo upande wa chama, si upande wa wagombea”

Kuhusu wanaoachia nafasi zao na kuusaka ubunge, Dkt. Bashiru amesema:

"Na ndiyo maana hairuhusiwi mtu anayegombea kushiriki katika vikao. Naomba nitaje jambo ningependa mtusaidie. Kuna baadhi ya wenyeviti wetu wa mikoa; sasa hivi wamefikia watatu -- mikoa mitatu. Wanaopaswa kukaa kwenye vikao vya kamati za siasa za mkoa (ndiyo wenyeviti); Kamati ya Usalama na Maadili (ndiyo wenyeviti); Halmashauri Kuu ya Mkoa (ndiyo wenyeviti). Sasa wameamua wao waache kiti wajadiliwe badala ya kuwajadili wengine. Na wakati wanaomba uongozi walikabidhiwa dhamana ya kusimika uongozi madhubuti wa kukiletea chama ushindi. Sasa wamaemua kuingia kwenye foleni ya kujadiliwa."

Kanuni yetu inasema:

Mwanachama atakuwa na haki ya kugombea nfasi yoyote ya uongozi lakini edapo kugombea nafasi nyingi kutasababisha kuzorota kwa uhai wa chama, hatateuliwa.

"Una haki ya kugombea lakini vikao vikisema wewe unafaa zaidi kuwa mwenyekiti, na ukitoka kwenye uenyekiti mkoa utayumba, sasa unafaa uenyekiti kuliko ubunge, unaweza ukaambiwa kaa kwenye uenyekiti kwa maslahi ya chama na uhai wa chama. Na wanajua hayo hao viongozi wetu."

“Ukishakuwa kiongozi hutakiwi kuwa na tamaa, ndiyo ujumbe Mwenyekiti ametuambia. Unatakiwa kutosheka, na ni moja ya sifa za kiongozi. Tosheka na dhamana uliyopewa na ukamilishe hiyo dhamana, upimwe kwadhamana hiyo – siyo unatangatanga tu.”

“Ni haki yake, ni haki yake; lakini ajue angepimwa vizuri kwa ngazi yake ya ukuu wa Mkoa. Najua baadhi ya wakuu wa mikoa ambao wamekaa kwa muda mrefu na majina yale utafikiri ni cheo yale. Nsa Kaisi watu wengine wangedhani kuna cheo kinaitwa Nsa Kaisi, lakini kwa kwasababu amekaa kwenye nafasi ile na ameitumikia kama Mkuu wa Mkoa.”

“Kuna mtu unakuta ndani ya miaka mitano tu kapata vyeo vikubwa viwili kwa mpigo alafu kabla hajakomaa pale, anataka ubunge. Ni haki yake lakini ni vizuri kujitathmini na kujitafakari.”

Msimamo wake wa kutogomea nafasi yoyote

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Dr. Bashiru Ally Kakurwa ameweka wazi msimamo wake wa kutogombea nafasi yoyote katika Chama hicho kwani ameridhika na nafasi aliyonayo.

“Mimi sigombei na siwezi kugombea, nimeshakuwa Katibu Kuu nagombea cheo gani?, cheo gani cha maana kuliko kazi hii ya kusimamia haki katika Chama” Katibu Mkuu CCM, Dkt.Bashiru

“Ukishakuwa kiongozi hutakiwi kuwa na tamaa ndio ujumbe Mwenyekiti ametuambia, unatakiwa kutosheka ndio moja ya sifa za kiongozi, tosheka na dhamana uliyopewa na uikamilishe hiyo dhamana na upimwe kwa dhamana hiyo sio unatangatanga tu” Dkt. Bashiru Ally

Anabweka tu hawezi kumkata makonda.
Mqkonda yupo strategically
 
Makonda,Ole sendeka,Gambo na katambi[emoji1787]safari imewakuta,Tamaa za uongozi zimewaponza[emoji38][emoji38]
 
CCM kila kitu wanafanya kwa maslahi ya mwenyekiti na chama, hakuna sehemu utaona wanasema kwa maslahi ya watanzania. A gang of wicked selfish monsters wanajali matumbo yao tu. Nchi iko palepale haiendelei. Africans kazi ipo sana kutoka kwenge umaskini sio leo wala kesho kwa akili za kishenzi hivi

Artificial intelligence naona matusi na kebehi kwa Waafrika yamekutoka bila sababu ya msingi! Wewe mwenyewe hapo uliyebahatika kupata elimu na maisha mazuri kidogo una ndugu zako wengi tu wanasota huko kijijini! Halafu leo unakuja hapa na dharau na kebehi kwa Waafrika wenzio kumbe hata wewe ni wale wale. Kwa dharau na matusi hayo akili hizo za kishenzi anazo nani?
 
Back
Top Bottom