denooJ
JF-Expert Member
- Mar 31, 2020
- 18,509
- 68,228
Kuongoza nchi sio sawa na kusukuma gari bovu ukiwa ndani, kuongoza nchi ni kupokea mawazo sahihi na kuyafanyia kazi, zaidi ni kuondokana na mawazo mgando yaliyotukwamisha tulipo na tulipotoka.Anapambana na nani? Bado yupo kundini na ubunge wa bure kapewa,
Atoke ajiuzulu ubunge, awe huru, huwezi kusukuma gari bovu ukiwa ndani,
Kwanini ufikirie anapambana na mtu? hii kwangu ni dalili ya uoga naona unaanza kujihami, Dr. Bashiru anaacha akili yake ifanye kazi kwa kuangalia namna bora atakayolisaidia taifa kusogea, huu sio mpambano wa uadui, ni mpambano wa kuleta maendeleo ya nchi.
Sioni kwa nani unamfukuza bungeni wakati bunngeni pia ni jukwaa la kutoa mawazo na yakasikilizwa na wengi, muhimu ni wale wanaoshauriwa kuwa tayari kubadilika, wala sio lazima Dr. Bashiru atoke bungeni ndio atoe mawazo yake, aachwe huru atoe mawazo yake kama ilivyo kwa kila mmoja wetu kwa nafasi yake kuanzia mitandaoni.