Nazgur
JF-Expert Member
- Apr 19, 2020
- 3,729
- 2,851
Hizo sera za majimbo muda wake bado sana hapa tanzania,Hii kauli ameisema Tundu Lissu mara mbili akimhusisha Bashiru Ally Katibu mkuu huyu wa ccm...
Mosi ni pale Bashiru alipomdhihaki Mh Lissu juu ya sera yake ya Uhuru akirudia alichokisema Mkapa 2015 akisema Tanzania tayari iko huru kwa nini lissu anazungumzia Uhuru?
Hizo Sera za majimbo muda wake bado SaNA hapa tz
Bila ajizi na bila kupepesa Mh Lissu akitumia kipawa chake cha hali ya juu akamfundisha Bashiru na watz maana ya Uhuru akimnukuu Baba wa taifa kwenye kitabu chake cha Uhuru na Umoja alichokiandika baara ya tz kupata uhuru 1961. Lkn pia alirejea azimio la tz kuingiza kwenye katiba yake maswala ya Uhuru na haki za binadamu ambalo nalo lilikuja baada ya Tanzania kupata uhuru.
Pili ni pale Bashiru alipoiponda sera ya majimbo ya Mh Tundu Lissu na chadema. Km kawaida mbeba maono huyu mwenye uwezo mkubwa na kushawishi na kujenga hoja hakusita kumshangaa Bashiru hasa kiwango chake cha akili anachokionyesha baada ya kuwa katibu mkuu wa chama dola ccm.....Akampa somo murua kabisa.
Ishu yangu ni je, Tundu Lissu anamaanisha nini anapomwambia Bashiru ana akili zaidi ya anazozionyesha?
Inamaana akiwa ccm anatumia akili zake kwa kiwango cha chini sn tofauti na awali alipokua mwalimu na mtu huru?
Je ni wangapi wapo km kina Bashiru wanatumia akili zao tofauti na zile zinazojulikana na wengi kwa vile tu wapo na wana vyeo ccm?
Check clip hiyo.... Je haya maoni ya Musiba kuhusu ili uwe mwana ccm ni lazima kua mnafiki wa kiwango cha phd yana ukweli?
NI KAULI YA KUFIKIRISHA. TUENDELEE KUTAFAKARI ZAIDI
Hilo likifanyika kuna mikoa mbayo ipo juu na itakuwa hivyo, na kuna mikoa ambayo ipo nyuma ma itabaki hivyo,
Hao magavana wataanza kubagua na kutoa pesa kidogo serikari kuu wakitaka kunyanyua majimbo yao sasa, mikoa ambayo haina rasilimali za kutosha itafanyaje?
Maana hao wananchi na magavana tutakuwa na nguvu ya maamuzi kwa mapato yetu hivyo hatutakubali pesa yetu itoke kujenga kungine wakati hatujalidhika na maendeleo tunayotaka.
Naongea hivyo si kwamba ninapoishi hakuana rasilimali,
Hapa tuna
Madini
Mbuga sehem kubwa
Ziwa sehem kubwa
Mpakani na nchi jirani
Hivyo kwetu hatuna shida na tutabana kweli hatutakubali ujingaujinga.