Bashungwa aongoza harambee ujenzi wa Ukumbi na Vyumba vya kulala Wageni Parokia ya Kasumo; zaidi ya milioni 45 zakusanywa

Bashungwa aongoza harambee ujenzi wa Ukumbi na Vyumba vya kulala Wageni Parokia ya Kasumo; zaidi ya milioni 45 zakusanywa

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
WhatsApp Image 2024-09-20 at 18.42.57_968d48eb.jpg
Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa (Mb) ameshiriki Misa Takatifu na kuongoza harambee ya kuchangia ujenzi wa ukumbi na vyumba vya kulala wageni katika Parokia ya Bikira Maria Malkia wa Amani Jimbo Katoliki la Kigoma ambapo zaidi ya shilingi Milioni 45 zimekusanywa.

Harambee hiyo imefanyika Mkoani Kigoma tarehe 20 Septemba, 2024 ambapo pamoja na mambo mengine, Waziri Bashungwa amemshukuru Baba Askofu wa Jimbo Katoliki la Kigoma Mhashamu Joseph Mlola kwa kumpa fursa hiyo ya pekee kushiriki Ibada ya Misa na kuongoza Harambee katika Kanisa la Kasumo ambalo umisionari wake ulianza mwaka wa 1985.
WhatsApp Image 2024-09-20 at 18.42.55_37c4ba15.jpg

WhatsApp Image 2024-09-20 at 18.42.52_90d3e075.jpg
Waziri Bashungwa amelipongeza Kanisa Katoliki Jimbo la Kigoma kwa uwekezaji wanaoendelea kuufanya pamoja na kutoa elimu bora kwa vijana katika Shule ya Sekondari ya Mtakatifu Rufino na Ronaldo na kuifanya shule hiyo kuwa na ufaulu mzuri.

Viongozi Wakuu waliochangia katika Harambee hiyo ni pamoja na Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Doto Biteko, Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba, Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, Naibu Waziri wa Maji Eng. Kundo Mathew, Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Eng. Maryprica Mahundi, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye pamoja na viongozi wengine wa Serikali.

WhatsApp Image 2024-09-20 at 18.42.51_980093c6.jpg

WhatsApp Image 2024-09-20 at 18.42.52_f9d4c4d2.jpg
Bashungwa amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuufungua Mkoa wa Kigoma na Mikoa ya Kagera, Tabora na Katavi kwa barabara za lami ambapo katika miradi inayotekelezwa mkoani humo Wakandarasi wanaendelea kufanya kazi usiku na mchana.

Akisoma Risala kwa niaba ya waumini wa Parokia ya Kasumo, Katibu wa Halmashauri ya Walei wa Parokia hiyo Bw. Onesmo Witae ameeleza kuwa hadi sasa wameweza kukusanya zaidi ya Shilingi Milioni 62 kutoka kwa wadau na marafiki wa Parokia hiyo kwa ajili ya ujenzi wa ukumbi na vyumba vya kulala wageni katika Parokia hiyo.
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2024-09-20 at 18.42.54_232bf93d.jpg
    WhatsApp Image 2024-09-20 at 18.42.54_232bf93d.jpg
    257.1 KB · Views: 8
Back
Top Bottom