Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,681
- 8,887
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Karagwe, Innocent Bashungwa amesema Bandari ya Dar es salaam haiuzwi na wala haibinafshwi na kwamba maamuzi ya Serikali kuhusu DP World kuendesha Bandari hiyo ni mkakati wa kupanua wigo wa vyanzo vya mapato ili kuondoa usumbufu kwa Wananchi kwa kutozwa tozo nyingi ambazo zingetumika kutekeleza miradi mbalimbali.
“Lazima tupanue wigo wa vyanzo vya mapato ili tusiwe tunaenda kwa Mwananchi huyohuyo kila siku tunaongeza tozo, tozo, tozo lazima Serikali iwe bunifu kwa kuangalia vyanzo ambavyo vitakuwa rafiki kwa Mwananchi kwa maana havitomrudisha nyuma kwenye umasikini kwa kumtoza zaidi kile ambacho anakipata kama pato na riziki yake”
Bashungwa amesema hayo wakati wa mwendelezo wa ziara yake Jimbo la Karagwe ya kuongea na Wananchi na kukagua miradi ya maendeleo katika Kata za Chonyonyo, Chanika, Rugera na Kihanga.
“Tanzania tuna Bandari ambayo ufanisi wake ulikuwa mdogo katika uendeshaji, ndio maana Serikalk ikaamua kutafuta Mwekezaji ambaye ataongeza ufanisi ili tuweze kupata mapato zaidi ambayo yataenda kutoa huduma za kijamii kwa Watanzania”
Bashungwa amewatoa hofu Wananchi wa Mkoa Kagera kwa kueleza kuwa Bandari haiuzwi wala haibinafishwi bali Serikali inaleta Mwekezaji ambaye ataiendesha kwa makubaliano yatakayoongeza ufanisi kiutendaji “Tumepata Mwekezaji ambaye ni kama unamkodisha kwamba nakupa duka langu lakini masharti ya uendeshaji ni moja, mbili, tatu”
Millard