Magical power
JF-Expert Member
- Sep 27, 2022
- 2,158
- 5,626
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kesi kubwa Sana hii.BASI BWANA!
Jana usiku kuna jirani yangu amegombana na mke wake. Yalikuwa majira ya usiku mwingi kidogo, nadhani wengi walikuwa wamelala.
Sikutoka nje, lakini niwe mkweli. Sikuziba sikizi lau moja. Nilisikia kila walichokuwa wakijibizana. Hata ilipofika zamu ya mke kupigika, nilisikia sauti ya makonde na namna alivyokuwa akiomba poo.
Kwa experience yangu ya kutengeneza tukio kwa kusikia. Niliweza kufahamu sababu ya ugomvi ule.
Ngoja niwasimulie.
Ilionesha mke amemsaliti mumewe kwa kutembea na mwanaume mwingine, ambaye pia ni mume wa mwanamke mwenziwe.
Pengine hii haikuwa issue iliyomuumiza yule mwamba.
Ishu ni msg ambayo mume ameikuta kwenye simu ya mkewe. Jamaa alisema kwa kulalamika, "Kwahiyo ukaona haitoshi ukaamua umwambie nina maumbile madogo!"
Hii ina maana gani?
Mke alimwambia huyo mwanaume kwa msg, kuwa mumewe hamtoshelezi. Maumbile yake hayafikii kete.
Kauli hii ilinifanya nijitazame na mimi. Nilisikitika sana na kuingiwa unyonge muda huohuo.
Mimi na huyo aliyenangwa tumetofautiana umri tu. Hayo yaliyotajwa kwa jina la maumbile, hadi najihurumia.
Lakini kuna haja gani ya kutangazana madhaifu?
Mnakera bhana.