Basi Kampuni ya Kapricon (T 605 DJR) iliyokuwa ikitokea Jijini Dar es Salaam kuelekea Arusha lapata ajali

Basi Kampuni ya Kapricon (T 605 DJR) iliyokuwa ikitokea Jijini Dar es Salaam kuelekea Arusha lapata ajali

Pdidy

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2007
Posts
57,951
Reaction score
32,619
#HABARI Watu wanne wamepoteza maisha na wengine 15 Kujeruhiwa baada ya basi Kampuni ya Kapricon (T 605 DJR) iliyokuwa ikitokea Jijini Dar es Salaam kuelekea Arusha kupata ajali ya kuacha njia na Kupinduka katika eneo la Maili kumi, barabara ya Segera-Korogwe mkoani Tanga.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga ACP Almachius Mchunguzi amesema ajali hiyo imetokea Octoba 3, 2024 majira ya saa 7 na nusu usiku, ambapo basi lilikuwa likiendeshwa na dereva aliyefahamika kwa jina la Julias Mushi (43) mkazi wa Arusha.

Kamanda Mchunguzi ametoa onyo kwa madereva kufuata Sheria za barabarani nyakati zote kwa kuchukua tahadhari na kuheshimu sheria za usalama Barabarani kuanzia mwanzo wa safari hadi mwisho wa Safari.

#EastAfricaRadio
 
Ty

Na nyie mna moyo gari yenyewe mkiangalia tu mimba bovu kabisa sijui n bei ndogo ama
Anyway rip
Na poleni
 

Attachments

  • 1727948076683.jpg
    1727948076683.jpg
    347.9 KB · Views: 5
Ty
 

Attachments

  • 1727948437281.jpg
    1727948437281.jpg
    171.3 KB · Views: 5
WATU wanne wamefariki dunia na wengine 15 kujeruhiwa baada ya basi walilokuwa wanasafiria la kampuni ya Kapricon kuacha njia na kupinduka.

Ajali hiyo ilitokea leo (Alhamisi) majira ya saa 7:30 usiku katika eneo la Mailikumi, wilayani Korogwe mkoani Tanga na kuhusisha basi lenye namba za usajili T 605 DJR.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Kamishna Msaidizi, Almachius Mchunguzi, amesema basi hilo lilikuwa linaendeshwa na Julius Mushi (43), Mkazi wa Arusha.

"Tumefuatilia na mpaka sasa waliopoteza maisha ni wanne ambapo wanaume watatu, mwanamke mmoja na wengine 15 wamejeruhiwa, majeruhi wanapatiwa matibabu katika hospitali ya Wilaya (Magunga) lakini wengine wamepelekwa katika Hospitali ya Rufani ya Mkoa ya Bombo," amesema.

Kamanda Mchunguzi alitoa wito kwa madereva kuwa makini wakati wa kuendesha Kwa kufuatia sheria za barabarani ili kuzuia vifo na majeruhi ambayo vinaweza kudhibitiwa.
#Nipashe
 
Kaprikoni bus, ni kampuni hatari kwa kuwa na magari mabovu!

Abiria epukeni kampuni hii, ma serikali isipochukua hatua, wengi watapotea!
 
Madereva wa mabasi makubwa ni wahuni tu.

Hakuna mwenye akili timamu.

Huwa wanaendesha magari kama wehu.
 
Ajali za Barabarani ni janga Dunia nzima.
 
Back
Top Bottom