Wanabodi,
Kwa ufupi ni route ya musoma-mwanza. Basi tajwa limenoa nanga saa kumi na moja unusu jioni kuelekea mwanza ambapo kituo cha mwisho inapaswa iwe buzuruga stand.
Changamoto ni gari kuharibika, limeharibikia sheli moja kisesa( mtanirekebisha wenyeji sheli inaitwa "wave").
Ameskika konda akisema "abiria shukeni mchimbe dawa chap."
Tukajua anakunywa mafuta safari iendelee, kumbe ni break down. Karibia dakika thelathini ikabidi abiria kuhoji. Kumbe gari imeharibika.
Abiria wana mizigo mizito, wanafikaje buzuruga na eneo sheli hapo ni mbali na vituo vy daladala? Je nauli ya kufika stendi ya buzuruga analipa nani?
Na kwanini isitolewe taarifa ya gari kuharibika?
Ni maswali aliyoulizwa konda, konda hakua n jibu wala hata kuomba samahani. Kilichofuata ni kama alimpigia simu bosi wake amtumie hela mpesa awalipie abiria wafike buzuruga.
Bana wee, konda akawa kama vile kazunguka upande wa pili wa gari, kumbe katoroka.
Wakawatelekeza abiria na kuacha gari wazi.
ABIRIA WAKAENDA POLISI HAPO KISESA
Wamekutwa askari wawili nje, wamepewa stori nzima na tiketi ya uthibitisho. Kufupisha stori afande mmoja kipara aliyeko zamu muda huu kasema," abiria rudini sheli kapigiwa trafiki anakuja hapo, lakini jiongezeni, tumieni akili zenu, mnaweza kuendelea na safari, hao watu wa basi watawasumbua."
HASIRA ZIKAWAKA
Abiria tayari hawana hela, wametelekezwa, wamepeleka shida zao polisi na polisi hawana msaada, je, wakalilie wapi?
Je, polisi na africa raha express wamekula mbinu kuwakomoa abiria?
Ni kwanini africa raha wajiamini namna hii?
Kwanini polisi wanashindwa ku enforce law kama jeshi? Ilhali nguvu zote wanazo? Wanawake na abiria wenye watoto wadogo usalama wao u juu ya nani?
MAMLAKA HUSIKA, TAFADHALI, TOENI ADHABU IWE FUNZO KWA WATU WA NAMNA HII ILI TABIA ZA NAMNA HII ZISIJIRUDIE.
USIKU MWEMA.