Basi la Africa Raha Express (T 382 DCS) latelekeza abiria sheli

Mleta mada ameweka concerns
  1. Kuna watu hawana nauli ya kufika stand
  2. Kuna watu wana mizigo mizito
  3. Mkataba wa abiria na mtoa huduma ni kuwafikisha stand, kama hawajafikishwa basi ni bovu, watafutiwe means ya kufika

Nakazia mjumbe.... Na hiki ndicho kinanifanya nielewe kwanini kiongozi yeyote wa nchi akiamua kufanya upumbavu wowote anafanya kwasababu keshajua wananchi wengi ni misukule. At all, watu hawalingani vipato. Kuvunja mkataba ni kosa kisheria.

Nimekuja kuonesha kosa ili wenye mamlaka wachukue hatua kama funzo kwa wengine ila kuna narrow minded people hata hawaelewi agenda kubwa ni ipi.

Acha kodi ziwekwe kede kede. At all mafuta yapande bei, tunaumia sisi so viongozi wa serikali, tozo za mihamala zinatuua sisi si serikali ambapo wao hadi communication allowances wanapewa.

Wananchi tuzinduke kama kenya hapo tuu muone kama viongozi watafanya upumbavu.

Nawaibia siri, nchi ya demokrasia, nguvu kamili iko kwa wananchi. Amkeni.
 

Ndio watanzania hawa, jamani tuwaombee. Kipindi flani niko chuo tunafanya mgomo, kuna watu kama wewe walijikuta wapenda skuli. Wenzao wakasusia pepa, yeye kaenda kufanya.

Akichapwa mboko hatokuja kusahau, lakini pepa alifutwa tukafanya wote fresh paper baada ya ndalichako kama waziri mwenye mamlaka kuingilia kati.

Yaani hujaona kabisa concerns hapa?
 

Ndugu, mimi nilikua kwenye tukio. Sumatra(latra) anasema gari likiharibika abiria asipewe taarifa?

Anasema gari akiaribika dereva na konda wakimbie wawatelekeza abiria?
 
Ri mjusi....ri reptilia
 
Upo uwezekano polisi na LATRA wakaenda kunufaika na hilo tatizo
 
Acha kulia lia kama mtoto hakuna polisi case hapo hayo ni mambo ya madai
 
Ofisi ya mtendaji kwanza haina mamlaka ya kufungua kesi na kitu ulicho fanya kufungua side mirror za gari ya watu huo ulikua ni wizi ungekutana na watu waelevu ungejutia kitendo ulicho fanya maana tayari ulisha jichukulia sheria mkononi.

Utakuja kulipishwa vioo vya gari yote siku moja, we utasema unadai 10k wao watasema ulifungua vitu vyenye thamani ya 1M na ushahidi ni hiyo side mirror uliyoenda nayo kwa huyo mtendaji asiejielewa
 
Ubaya zaidi hata Sisi Humu JF wengi hatuwezi saidia. Matatizo ya Nchi Yetu Ni Umasikini
 
Kama wanaume mpo hao ng'oeni hizo tairi za nyuma nakuja chap na mteja anayo cash atawapa pesa ya nauli. Huyo mmiliki wa pesa ile pesa ya kuwarudishieni mfike stand akanunulie tairi.
 
Sikilizeni, kama bus imeachwa hapo, fanyeni utaratibu wa kuuza matairi, taa, tank ya mafuta, engine, shock absorber, gearbox, vioo, siti, chassis na vyengine wao waachieni funguo tu apo sheli
Huo ni wizi sasa watapata pesa zaidi ya nauli yao tairi tu za nyuma tu kwa bei ya hasara wanapata milioni,inawatosha kufika stand.
 
Chomeni moto hilo basi lao mkweche iwe fundisho kwa wangese wengine.
Basi la milioni 300 uchome moto kwa nauli isiyozidi milioni.
Boss muungwana anaetegemea akili na sio ndumba kuendesha biashara,fasta hapo angekodi daladala akampa elf 50,abiria wote wangefika stand kuu.
Mizigo mizito utasubiria gari itengenezwe.
 
Nenda kwa DC au RC wa eneo hilo.
 
Mfanyabiashara kumwacha Mteja ananung'unika ni kosa kubwa sana. Unajiharibia biashara yako mwenyewe..

Nina uhakika abiria 50 waliomo kwenye hilo Basi hawatathubutu tena kurudia kupanda mabasi ya Kampuni hiyo..

Wafanyabiashara wengine wanachokifanya, huita Costa mbili na kupatana nao wawasogezee Abiria stand.. Isitoshe Kisesa - Buzuruga siyo umbali mrefu kiasi cha kukimbia Jukumu la kumfikisha Abiria kwenye final destination..
 
Basi la milioni 300 uchome moto kwa nauli isiyozidi milioni.
Boss muungwana anaetegemea akili na sio ndumba kuendesha biashara,fasta hapo angekodi daladala akampa elf 50,abiria wote wangefika stand kuu.
Mizigo mizito utasubiria gari itengenezwe.
Usilinganishe thamani ya basi na utu wa mtu.
Wakichoma moto hilo basi next time mwenye basi atakuwa na akili timamu.
 
Muwe mna angalia na ma bus ya kupanda hilo bus lina onekana tu ni choka mbaya
 
Sitasahau safari yangu kutoka lindi mpaka Dar. Ilikuwa yamateso
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…