Manyema
JF-Expert Member
- Sep 2, 2010
- 683
- 1,801
Kuna siku nilikuwa natoka Arusha kuja Dar na bus la BM coach, baada tu ya kupita Mombo pale mbele kidogo karibu na ile hotel ya Kilimanjaro tukasimamishwa. Jamaa wako na defender 2, wakaanza kusearch bus walisearch vibaya mno fungua buti zote wanamaliza wanarudia tena, walitumia kama dk 45 hivi hadi abira tukaanzisha kama zogo hivi lakini hawajali. Ila bahati nzuri hawakukuta chochote wakatuachia kwa shingo upande unaona kabisa kama hawajaridhika. Nadhani aliyewapa mchongo atakuwa alikosea namba ya gari maana Chuga BM zinatoka nyingi za kutosha, hivyo tukaendelea na safari yetu sema walituchelewesha sana.