Tetesi: Basi la Tabora One latekwa kwenye pori kati ya Itigi na Tabora usiku wa jana

Tetesi: Basi la Tabora One latekwa kwenye pori kati ya Itigi na Tabora usiku wa jana

Yameanza tena hayo majambazi, basi yakae mkao wa kunyolewa sasa hivi.
 
Mbaya sana kama ujambazi huo umerejea.Duu Tabora One anapigwa vita sana njia hiyo ya tabora na mmiliki mkongwe wa njia hiyo,pia mmiliki wa tabora one alifariki miezi michache iliyopita basi ni balaa tupu.Waliobaki wasikate tamaa
Nani mkongwe barabara hiyo mkuu
 
Dah..mkuu...mie nadhani polisi wangeacha kwanza kusumbuana na wakina tundu lissu...badala yake wakafanye operesheni nzito ya kuwanasa hawa majambazi. Itakuaje wananchi wanakosa uhuru wa kusafiri usiku kwenye nchi yao? Africa mashariki yote hii wenzetu wanasafiri...ni sisi tu hili wimbi la majambazi limetushinda mpaka tumezuia safari za usiku. Inasikitisha sana
Mabasi yalikatazwa kusafiri usiku... Maybe madereva wana michongo na majambazi kuwajaza kingi wasafiri usiku
 
Mbaya sana kama ujambazi huo umerejea.Duu Tabora One anapigwa vita sana njia hiyo ya tabora na mmiliki mkongwe wa njia hiyo,pia mmiliki wa tabora one alifariki miezi michache iliyopita basi ni balaa tupu.Waliobaki wasikate tamaa
acha porojo. unauhakika na haya unayoyasema?
 
Mabasi yalikatazwa kusafiri usiku... Maybe madereva wana michongo na majambazi kuwajaza kingi wasafiri usiku

Ofcourse nafahamu kwa sasa safari za usiku haziruhusiwi..na inabidi iwe hivyo mpaka usalama ukae vizuri. Ila ninachosema hatuwezi kudumu kwa hali hii mkuu. Yani nchi huru yenye jeshi la polisi...wananchi wake wanyimwe uhuru wakusafiri muda wowote wanaotaka eti kwasababu majambazi yametamalaki? Hii sio sawa. Ifike mahali polisi wafanye operesheni kali ya kuwamaliza hawa jamaa...lasivyo hatuna haja ya kujivunia kuwa na vikosi vya usalama.
 
Ukitaka askari wafike haraka eneo la tukio,wapigie kuwa UKAWA wanataka kuandamana.
Duh! Nilikuwa sijacheka tokea asubuhi, hii imenifurahisha na kumalizia siku.
 
Kilo mita ni sawa labda wingi wa abiria ila hio njia ya itigi manyoni tabora inatisha nilitembea masaa ma 4 network ya simu hamna
Kijana acha ubishi wewe.
Tabora dsm via nzega na tabora -dsm via itigi ni kanisa na msikiti.
Tofauti kabisa.
Unaujua umbali wa kutoka itigi -tabora na umbali wa kutoka mkiwa..(nje ya mji wa manyoni) to tabora???
 
Kuna taarifa kuwa Basi la Tabora One lifanyalo safari zake kati ya Dar na Tabora, limetekwa Jana usiku na abiria wote kunyang'anywa mali zao na kuna taarifa kuwa huenda wanawake wamefanyiwa vitendo vya ubakaji.
aisee siwangewabaka wanaume kwa nini wawaonee wanyonge kinamama zetu
 
Mabasi yalikatazwa kusafiri usiku

Haya yote yanatokea kwa kutofuatwa sheria.Sheria ipo ingawa nayo kwangu naiona ina mapungufu.Sheria inadai mabasi ya abiria kutosafiri baada ya saa nne usiku na badala yake yaegeshwa kwenye miji usiku ulipolikuta basi.Mimi ningeshauri wizara/mamlaka husika kuirekebisha hii sheria kwamba mara tu ifikapo saa 12.30 jioni basi lolote la abiria lisiruhusiwe kuendelea na safari hadi kesho yake asubuhi saa 12. Walisema wahenga usiku haushoni nguo wakiwa na maana maovu mengi hutendeka usiku.Utekaji wa magari,wizi kwa abiria na unyanyaswaji kina mama hufanyika usiku.Pia ajali za usiku zina matatizo.Abiria au gari linaweza kurushwa mbali na barabara au kuangukia bondeni na isifahamike mapema hivyo abiria kuvuja damu muda mrefu na kufariki au hata kulaliwa na gari.Usiku sio rahisi magari kusimama kutoa misaada kwa kuhofia usalama wao.Ni wakati sasa kama ni Ewura au wizara kuiangalia upya hii sheria.Lipo pia tatizo la matajiri wa mabasi hayo kuwaamuru madereva wao kusafiri usiku ili asubuhi gari hilo hilo lianze safari upya.Gari hazipati matengenezo baada ya safari ndefu.Ni matajiri wachache sana na wenye magari mengi wanaoipumzisha na kuifanyia matengenezo gari iliyotoka safari ya mbali.Kwa upande wa abiria nao wamkataze dereva kuliendesha gari usiku kwa wao kutaka kuwahi makwao au biashara zao huku wakijua kinachoenda kuwapata usiku ni kutekwa au kuanguka maana usiku gari hukimbizwa sana kwa kutowepo askari barabarani.
 
Back
Top Bottom