Basic math test that most people get wrong

Basic math test that most people get wrong

👏👏👏Basic accounting, revenue minus expenses = gross profit.

Na hapo ndio watu wa mtaani wanapotengeneza pesa na kufanikiwa kwenye biashara kuliko wazee wa accounts.

Hiyo formula au hesabu haisemi alipata wapi USD 10 ya kuongeza kwenye USD 70 ili ifike USD 80 ya kumnunua tena huyo mbuzi.

Ikumbukwe tunaongelea faida aliyoipata Kwa muamala wa huyo mbuzi tu.
 
[emoji122][emoji122][emoji122]Basic accounting, revenue minus expenses = gross profit.
Hesabu ni janga la kitaifa.
Kwa wale wenzangu na mimi ambao hatuhitaji kanuni za pythagorus;

*Msichanganywe na kuwa mnunuzi wa kwanza alijitokeza zaidi ya mara moja. Fanya kama wanunuzi wangekuwa wawili tofauti

*Usichanganywe na wapi ilipatikana 80 wakati mauzo ya awali na faida ikiwemo ilikuwa 70. We waza tu kuwa jamaa alikuwa na pochi nene akaamua acheze patapotea. Kimsingi ugumu wa hesabu unakolezwa na maelezo yanayojikanganya
 
1st round
Buying price $60
Selling price $70
Profit= $10

2nd round
Buying price $80
Selling price $90606
Profit =$10

Total Profit= $20
Dola 60 akauza 70 faida 10....
Akamnunua tena kwa 80 inamaanisha ile 10 ya faida imepotea.... hiyo tunaita bilabila
Kamuuza kwa 90 maana yake kapata tena 10

Faida hapo ni dola 10. Mimi ni jiniaz wa hesabu, baraza la mitihani wananijua.

Mi kinachonishangaza kwanini huyu mbuzi auzwe kwa dola? Mbuzi wa kununuliwa kwa dola atakuwa na supu tamu?
 
1. Kanunua $60
2. Kauza $70, faida $10
3. Kanunua $80, hasara $10
4. Kauza $90, faida $10, akifidia hasara hapo juu ya $10 hana faida.

Biashara kichaa. Kabaki kama alivyoamka na $60 yake
Utasemaje aliponunua kwa 80 alipata hasara wakati aliiuza kw 90 baadae?

Hasara inakuwa determined kwa mauzo ya baada ya kununua, sio mauzo ya kabla hujanunua,

Alinunua 60 kisha baada ya kununua akauza kwa 70 ( mauzo -manunuazi ni 70-60)

Kisha akanunua kwa 80 na kuuza kwa 90 ( mauzo -manunuzi ni 90-80)

Huwezi kutafuta hasara kwa kuchukua manunuzi ya sasa kisha utoe na mauzo ya kipindi kilichopita, unatoa na mauzo utakayouza
 
Dola 60 akauza 70 faida 10....
Akamnunua tena kwa 80 inamaanisha ile 10 ya faida imepotea.... hiyo tunaita bilabila
Kamuuza kwa 90 maana yake kapata tena 10

Faida hapo ni dola 10. Mimi ni jiniaz wa hesabu, baraza la mitihani wananijua.

Mi kinachonishangaza kwanini huyu mbuzi auzwe kwa dola? Mbuzi wa kununuliwa kwa dola atakuwa na supu tamu?
Mbona hata chupi inauzwa kwa dola??
 
Tuanze

1. Kanunua mbuzi wa 60

2. Kamuuza kwa 70 maana yake ni kapata faida ya 10=(70-60)

3. Kamnunua tena kwa 80 maana ake kama alimuuza kwa 70 na kamnunua tena kwa 80 hivyo hata ile faida ya 10 haitaonekana hivyo itabidi aongezee 10 nyingine ili iwe 70+10=80ya kumnunu upya,
hivyo hapa ana hasara ya 10
(Weka kichwani hapa hasara ya 10=-10)

4. Kamuuza tena kwa 90 hivyo kapata faida ya 10=90-80

Hitimisho
Kumnunua mbuzi kwa mara ya pili aliingiza hasara ya 10 na kwenye kumuuza kwa mara ya pili kapata faida ya 10 basi alichokipata ni 10+-10=0

bas hakuna alichokipata.
Kifupi ni biashara kichaaa🤣
Wewe ni jiniaz. Lazima unatumia K Vant wewe....
 
Alikua na $70 mwanzo, kaishia na $90 mwisho
 
mbona hata chupi inauzwa kwa dola??
Afadhali chupi inafunika sehemu nyeti. Sasa huyu mbuzi nyeti yake anaiweka wazi kabisa na mkia anaunyanyua juu utamnunuaje kwa dola huku Mpitimbi?
 
1. Kanunua $60
2. Kauza $70, faida $10
3. Kanunua $80, hasara $10
4. Kauza $90, faida $10, akifidia hasara hapo juu ya $10 hana faida.

Biashara kichaa. Kabaki kama alivyoamka na $60 yake
Huyu Mwamba katengeneza $20 fasta. Assune yuko na $100, akamnunua Mbuzi kwa $60, akamwuza kwa $70. Hapo katengeneza $10. So mshiko wake unakuwa $110. Akajizungusha, akatudi tena akamnunua kwa $80, kwenye ile $110 ikabaki $30. Akamwuza kwa $90. $90+$30= $120.
Mwamba ameingiza $20 Chapchap.
 
Dola 60 akauza 70 faida 10....
Akamnunua tena kwa 80 inamaanisha ile 10 ya faida imepotea.... hiyo tunaita bilabila
Kamuuza kwa 90 maana yake kapata tena 10

Faida hapo ni dola 10. Mimi ni jiniaz wa hesabu, baraza la mitihani wananijua.

Mi kinachonishangaza kwanini huyu mbuzi auzwe kwa dola? Mbuzi wa kununuliwa kwa dola atakuwa na supu tamu?

Hapo kwenye kusema wanunuzi wangekuwa tofauti unakosea

Kwenye Maths zipo kanuni za AND na OR

Kwasababu mnunuzi ni mmoja maana ake inatumika AND

ila wangekuwa wawili Tofauti zingetumika kanuni za OR

Sa wakiwa wawili tofouti basi kila mmoja angepata faida ya 10


Ila ya mmoja hakuna faida.
 
Na hapo ndio watu wa mtaani wanapotengeneza pesa na kufanikiwa kwenye biashara kuliko wazee wa accounts...
Mimi nipo mtaani, nimesoma accounts na nina practice in real life mtaani

Nafanya biashara ya nafaka sasa hivi, hii biashara leo mahindi yanaweza kuwa 600 kesho yakawa 700 kama huo mfano wa mbuzi

Mimi nanunua mahindi 700 shamba kisha naenda kuuza 800 sokoni, naweka faida mfukoni

Kesho naenda nakuta tena bei imebadilika mahindi yanauzwa 900, nayanunua 900 kisha naenda kuuza 1000 sokoni

Hapo hakuna hasara ninayopata hata nikinunua kwa bei ya juu kila kuliko niliyouzia kwa round iliyopita, cha muhimu ni kuhakikisha kwa kila round, bei nitakayoenda kuuza itakuwa kubwa kuliko niliyonunua

Ni hivyo hivyo kwa huyo mbuzi, round ya kwanza alinunua kwa 60 akauza 70 tayari ya kuuza ni kubwa kuliko ya kununua ni faida

Round ya pili akanunua 80 kisha akauza 90, hapo pia bei aliyouza ni kubwa kuliko aliyonunulia, so ni faida kila round
 
Mimi nipo mtaani, nimesoma accounts na nina practice in real life mtaani...

Umezingatia swali lililoulizwa? Umeambiwa katengeneza faida kiasi Gani kutokana na huyo mbuzi.

Kwa kuzingatia kwamba alikua na USD 60 tu kama mtaji.

Mfano ulioutoa ndio Hali ilivyo mtaani.

Sasa hapo faida ya USD 10 jumlisha na USD 60 aliyokuwa nayo inakua USD 70. Anatakiwa anunue mbuzi Kwa USD 80. Hapo inakuaje?
 
Back
Top Bottom