Wewe unaamini kwamba Bastola ndiyo itakulinda?
Kama Sio mtu wa Mambo ya Ulinzi Na Usalama , silaha unayomiliki kama hujaua nayo mtu basi itakuuwa wewe, yaani put that on note.
History inaonesha wazi Raia wengi wanaomiliki Bastola ni aidha Ina wamaliza au inamaliza wengine for no reason. Nina miliki Bastola lakini kwa sababu ya nature ya kazi yangu inanitaka hivo. Na kuna siku almanusura ilitaka kunimalizia kiumbe changu. I totally discourage mtu kumiliki Bastola kwa matumizi ya kawaida, eti kwa kigezo cha kulinda mali zangu nyumbani.
Bastola hailindi mali zako, watu wakiamua kukufanyia unyama wanakufanyia Na Bastola yako .... maana it is all about timing. Erasto msuya alikuwa na Bastola , ilimsaidia ?kila siku tunasikia polisi na wanajeshi wanapigana Bastola for no reason. Yaani mtu anakuja ofisi and Yupo desperate, anafika na kulipua wenzie, na haijulikani sababu ni nini. Ndiyo ipo Hivyo, ni vile tu haitakiwi kutangazwa. Lakini jeshini na polisi matukio hayo ni kawaida sana
Kwanza Bastola zenyewe mnazomiliki ni hizi za Taa, halafu inajikoki tena for more that 30sec, ndio usikie tena Taa ..yaani ina shout then Ina reload . .., wakati yako ina reload , mwenzio kashakupiga mwili mzima.
Ditopile aliulizwa, Dito kwa nini umemuua huyu maskini, alijibu kwa hakika hakukusudia kumuua bali alitaka kumtisha Tu, wakati ana knock kioo cha gari kwa kutumia Bastola, trigger ikajiset na kujiachia.... !
Bastola kama haijakuua basi utaua wengine hata kwa bahati mbaya. Na ukishaua mtu huwezi kuwa sawa sawa tena. Sishauri kabjsa kama Sio mtu wa ulinzi na usalama. Ishi vyema na watu, epuka wizi wizi, na ubishi ubishi usio na msingi, usiweke bifu na watu. Asilimia 80 yetu ni mania Bipolar , akiwa kwenye moody, atafanya kisha kujuta. Wengi wetu ni machizi wasomi so be careful