Bata ni mchafu lakini ni mtamu sana kuliko kuku

inabidi umuwekee viungo gani? kwa nini maandalizi yake ni muda mrefu?

Sent using Jamii Forums mobile app
Viungo ni kama vilivile tu unavyo weka kwenye nyama ya kuku,
Anachukua mda mrefu kwa sababu anavitu vingi vya kuvitengeneza na mwili wake ulivyo ni tofauti na kuku pia ata kumny'ony'oa ni kazi
 
Kipendacho roho sijawahi kuielewa nyama yake kwanza inakishombo fulani hata uweke ndimu haikati harufu.
Nyama ya bata Haina shombo! Ukiona shombo ujue umechemka kuiandaa! Haiandaliwi kama nyama ya kuku.
 
Duh! Nilikua napitia comments za wadau naona wengi wamecoment kuwa nyama ya bata ni tamu lkn hawajaeleza anaandaliwaje! Wengine wanadai nyama ya bata ina shombo lkn hawajui shombo linasababishwa na nn?

Nijuavyo mie:
1.Ukishamchinja bata wako, hakikisha unanyonyoa na maji ya moto kama kawaida tu.
2. Chukua pumba kiasi anza kumsugua kila eneo la mwili wake.
3. Chukua maji safi ya moto yaliyochemka 100c hayo ndio msuuze nayo, itapendeza zaidi kama ukirudia tendo hilo lkn tumia maji mengine kwa kumsuuzia nayo yawe ya moto kama Yale ya kwanza.

Kwa nn tumsugue na pumba na kumsuuza na maji ya moto?
Jibu. Kwa asili bata ana M'ba ktk mwili wake mithili ya ukoko ule ndio haswaa unaoleta shombo ktk nyama yake kama haujaondolewa vzr, nadhani hadi hapo tupo pamoja!
4. Kuna vinyoya kaidi vidooogo sana na kimoja kimoja hv vinaondolewa kwa kumbabua ktk moto, hapa tumia jiko la Mkaa na kuwe na wavu ili asichafuke, usitumie kuni, maana kuni itaharibu nyama kwa moshi.
5. Katakata nyama yako vizuri, hakikisha umeweka mchanganyiko wa vitu vitatu ktk hiyo nyama!
I. Chumvi
II.Tangawizi ambayo umeiblend.
III. Kamulia na limao la kutosha, acha nyama ichemke, usiweke maji, ile nyama itachemka hadi maji yake yenyewe yatakaukia.
6. Yale maji yakikaukia chini ya sufuria yatabaki mafuta ya kutosha tu! Punguza vipande ktk sahani ili vibaki vichache ktk sufuria vijikaange kwa urahisi na mafuta yake, hapa usiongeze mafuta yoyote yaliyopo ktk sufuria huwaga mengi na yanatosha, hakikisha vipande vya nyama vinakuwa Brown, then malizia na hivyo vingine navyo hadi vinakuwa Brown!
Baba, baba, baba kama nyama hiyo ipo ndani nakuhakikishia kila ukiingia lazima utafune kimoja[emoji23], hiyo hainuki shombo wala nn!
NB: Nyama hii haipendezi sana kwa mchuzi, kausha kama nilivyokuelekeza!
 
kweli we ni mtaalamu bila shaka amejifunza,yataka utulivu huyu ni bata.

Hujawai kusikia mtaani wakisema twende tukale kuku
Utasikia wakisema twende tukale bata
Iyo ni kumaanisha starehe na inamaanisha bata ni mtamu kuliko kuku
 
Viungo ni kama vilivile tu unavyo weka kwenye nyama ya kuku,
Anachukua mda mrefu kwa sababu anavitu vingi vya kuvitengeneza na mwili wake ulivyo ni tofauti na kuku pia ata kumny'ony'oa ni kazi
Hivi kwa nini ukishamaliza kumnyonyoa anatoa vinyoa vingine laini laini?
Nilishangaa sana mwezi ulioisha tuliandaa bata mimi na dada.
Dada akasema wakati wa kumnyonyoa usiongee ataota manyoya mie nikawa naongea.
Kweli bana kama utani tu naona manyoya yanaota.
Siamini sababu aliyonipa dada.
Lakini nilishangaa jamani
 
😂😂😂😂😂 kwamba usiongee!!!!!!!
 
Duh.....hi mpya kwangu mkuu
 
Back
Top Bottom