Battery yangu ya solar inaisha nguvu haraka

mkuu shukrani,kuna kitu nimejifunza hapa maana na mimi ni muhanga .Nimefunga solar ktk ofisi ila mda wote inahitaji support ya umeme wa tanesco kuzichaji battery na huwa hazikai kwa mda mrefu bila support ya umeme
 
Na wengine huwa wana-connect load pale pale zinapoungwa battery. Hii hufanya battery zisiwe disconnected na charger controller wakati battery imefika minimum voltage value, of which, if you go below that, utaiharibu tu... kwa waliosoma elesticity... ni sawa na mpira uunyumbue hadi uvuke plastic limit, halafu utegemee urudi kwenye original shape.. NO WAY
 
kama bado una hili tatizo,nunua Mobisol au solar za kampuni yoyote ambayo Battery limeungana na system yani huwezi kufungua battery ,yanakua na ubora sana haya,unaweza kutumia siku 2 bila moto kukata
 
P=IV, 11.25A*3hrs
 
Angalia level ya maji kwa kila week au mara moja kwa mwezi, ongeza distilled water mpaka kwenye level ya max, usiweke batteries chini/sakafuni au kwenye tiles
 
Hivi hakuna kifaa kinachoweza kubadili solar current ya DC kwenda AC!
Maana hii solar niliyofunga ni DC tu mpaka nashindwa kutumia vifaa vingine kama laptop!
Sijui mfumo gani huu wa solar sikuwahi kuushuhudia kabla! Inanipa shida kweli
Hata laptop inatumia Vdc mkuu, adapter inabadili Vac kwenda Vdc ndio unatumia kwenye Laptop yako.

Inverter ndio kifaa unachohitaji. Ukijitahidi kutumia mfumo wa 24Vdc ni nzuri kuliko 12Vdc, V=IR
 
Angalia level ya maji kwa kila week au mara moja kwa mwezi, ongeza distilled water mpaka kwenye level ya max, usiweke batteries chini/sakafuni au kwenye tiles
Baada ya kusumbuka sana nilinunua zile betrii za mobisol huu mwaka wa tatu hakuna usumbufu.
 
Msaada na kwangu wakuu..... nna panel ya 150 na betri dry n100 ya gari nikitumia charger control inaonekana kujaa kabisa lakini ukija kuwasha hata balbu moja tu haichukui hata dk 20 imeisha chaji.... ila ukiunga direct ni masaa manne tu nawasha balbu tano usiku kucha...... zamani nilivyofunga hii system nlikuwa nikiangalia tv mchana kutwa na usiku kucha nawasha balbu nne..... je tatizo inaweza kuwa nini?
 
Controller. Ila hapo uliposema ukiunga DIRECT unamaanisha nini, kuunga Panel direct kwenye batteries? Ni hatari kama huna ulinzi, panel itaondoka kimasihara tu.

Na kama ni kuunganisha hizo balbu direct kwenye batteries, ndio unapata masaa 4 ila ukipitia controller ni dk 20, tafuta tu controller nyingine.
 
Shukraan mkuu.... kuunga kwa maana ya kuunganisha moja kwa moja toka panel mpaka betri bila kutumia controller
 
Shukraan mkuu.... kuunga kwa maana ya kuunganisha moja kwa moja toka panel mpaka betri bila kutumia controller
Utaunguza hizo photocells za kwenye panel yako, waya kupata joto n.k Panel yako inatoa Volts ngapi? 12, 24, 36 au 48? Tafuta Diode ya saizi stahiki ufunge kwenye waya mwekundu.
 
Angalia level ya maji kwa kila week au mara moja kwa mwezi, ongeza distilled water mpaka kwenye level ya max, usiweke batteries chini/sakafuni au kwenye tiles
Mkuu, hata kama battery imeandikwa 'regulated lead acid' inawekewa distilled water? Vipi nikiweka maji makali ya battery?
 
Naunganishaje tv na king'amzi (vyote ni dc)katika mfumo wa betri na charger controla ili viweze kuwaka? Naunga kwenye terminal za betri au kwenye output ya sola controla
 
Nakubaliana na wewe betri nzuri dry ya ritar N100 mimi ninayo pia ina miaka mitatu lakini ndio inazidi kuwa strong, ila hapo kwenye solar panel umepuyanga, kioo cha watt100 hakina uwezo wa kujaza betri ya N100 kila siku Never. Hiyo betri itakuwa haijai, na at the end hiyo betri itakufa, kioo kinachoweza kujaza vizuri betri ya N100 ni kioo cha watt150, na hapo kwenye control 10amp ni ndogo inafaa 20amp. Yani ukifunga system yako kwa mpangilio huo maisha utayaona matamu sana. Nawasilisha
 
Naunganishaje tv na king'amzi (vyote ni dc)katika mfumo wa betri na charger controla ili viweze kuwaka? Naunga kwenye terminal za betri au kwenye output ya sola controla
Unachotakiwa kufanya unganisha waya kwenye betri terminals, halafu nunua twin socket kwisha kazi TV na kingamuzi vyote vitawaka
 
Mimi nina solar panel 200W. Nikinunua Battery ya 100W itaweza kujaa na kuwasha taa zangu 16? (4 zinawaka usiku mzima na 12 zinawaka mpaka saa 5 tu)
 
Mimi nina solar panel 200W. Nikinunua Battery ya 100W itaweza kujaa na kuwasha taa zangu 16? (4 zinawaka usiku mzima na 12 zinawaka mpaka saa 5 tu)
Hiyo panel kwa betri la n100 ni kutoitendea haki yake.
Kama una betri la n100 panel ya 120w inakutosha kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…