Tatizo, watu wengi wenye solar system, huwa hamzichaji hizo batteries to full charge.... na huwa mnazitumia mpaka baatery ya 12V inavika 8V... Ukiifikisha battery hapo, una-destroy cells. Zikishaharibika hutaweza kuzichaji tena to full capacity
Halafu anayekushauri ununue battery ya Ampare Hour kubwa (N100), je solar panels zako zina uwezo wa kuichaji hiyo battery?
Kumbuka, wakati wa mchana, jua linapokuwepo, solar panels, zinapeleka umeme sehemu mbili, mzigo wako (Taa, na vifaa vyote vinavyotumia umeme wa hiyo solar) na kuchaji battery. Sasa kama hesabu haijapigwa vizuri, hutakuja kuijaza hiyo battery, na utakuwa unaitumia kabla haijajaa kila siku, HENCE WITH TIME, ITAKUFA...