Battery yangu ya solar inaisha nguvu haraka

Battery yangu ya solar inaisha nguvu haraka

Tatizo, watu wengi wenye solar system, huwa hamzichaji hizo batteries to full charge.... na huwa mnazitumia mpaka baatery ya 12V inavika 8V... Ukiifikisha battery hapo, una-destroy cells. Zikishaharibika hutaweza kuzichaji tena to full capacity

Halafu anayekushauri ununue battery ya Ampare Hour kubwa (N100), je solar panels zako zina uwezo wa kuichaji hiyo battery?

Kumbuka, wakati wa mchana, jua linapokuwepo, solar panels, zinapeleka umeme sehemu mbili, mzigo wako (Taa, na vifaa vyote vinavyotumia umeme wa hiyo solar) na kuchaji battery. Sasa kama hesabu haijapigwa vizuri, hutakuja kuijaza hiyo battery, na utakuwa unaitumia kabla haijajaa kila siku, HENCE WITH TIME, ITAKUFA...
mkuu shukrani,kuna kitu nimejifunza hapa maana na mimi ni muhanga .Nimefunga solar ktk ofisi ila mda wote inahitaji support ya umeme wa tanesco kuzichaji battery na huwa hazikai kwa mda mrefu bila support ya umeme
 
Na wengine huwa wana-connect load pale pale zinapoungwa battery. Hii hufanya battery zisiwe disconnected na charger controller wakati battery imefika minimum voltage value, of which, if you go below that, utaiharibu tu... kwa waliosoma elesticity... ni sawa na mpira uunyumbue hadi uvuke plastic limit, halafu utegemee urudi kwenye original shape.. NO WAY
 
Habari wana jf?
Battery yangu ya solar imekuwa ikipoteza nguvu ndani ya masaa mawili baada ya kuwa full charged, ni battery ya maji (acid) na pia nimeshawahi kuiongezea maji(acid) mara mbili kwa kipindi tofauti ila hakuna improvement. Je kunautalam wowote naweza kufanya ikarudia hali yake hata kwa 50 -70%?. Nawasilisha hoja

kama bado una hili tatizo,nunua Mobisol au solar za kampuni yoyote ambayo Battery limeungana na system yani huwezi kufungua battery ,yanakua na ubora sana haya,unaweza kutumia siku 2 bila moto kukata
 
Fanya hivi mkuu chukuwa 115+20=120w
Then let say taa zote ni 15w
Jumla ni 135w
Hivyo basi ni betri size gani utahitaji?
Kama mfumo wako ni wa volt 12, chukuwa 135w÷12v=11.25ah
So wewe unataka angalau masaa 3 hivyo 11.25ah*3h =33.75ah
So utahitaji betri ya 40ah na pannel ya 50w

Mimi si mwalimu ila nauza solar syatem
P=IV, 11.25A*3hrs
 
Kuna pasi za solar zina watts 150, zile za umeme ni zaidi hapo hadi watts 1000 zipo.

------------------------
Mi naomba ufafanuzi wa betri la dry linatakiwa liweje, kuna siku nilienda dukani kununua betri nikaomba la dry nikapewa ambalo kwa ndani lina maji halafu kwa juu kuna tundu lililofunikwa na kioo kama lenzi nikalikataa, nikazunguka maduka mengi na wote wananipa ya hivyo hadi nikaamua kununua la kujaza maji ya acid.

Betri hili nimelitumia baada ya mwaka nikataka kubadilisha maji, baada ya kulifungua nikakuta maji yote yalikauka nikaweka mengine. Je, kiutaalam maji yanatakiwa yabadirishwe baada ya muda gani? Na kutumia hadi maji kuisha betri haliwezi kufa?
Angalia level ya maji kwa kila week au mara moja kwa mwezi, ongeza distilled water mpaka kwenye level ya max, usiweke batteries chini/sakafuni au kwenye tiles
 
Hivi hakuna kifaa kinachoweza kubadili solar current ya DC kwenda AC!
Maana hii solar niliyofunga ni DC tu mpaka nashindwa kutumia vifaa vingine kama laptop!
Sijui mfumo gani huu wa solar sikuwahi kuushuhudia kabla! Inanipa shida kweli
Hata laptop inatumia Vdc mkuu, adapter inabadili Vac kwenda Vdc ndio unatumia kwenye Laptop yako.

Inverter ndio kifaa unachohitaji. Ukijitahidi kutumia mfumo wa 24Vdc ni nzuri kuliko 12Vdc, V=IR
 
Angalia level ya maji kwa kila week au mara moja kwa mwezi, ongeza distilled water mpaka kwenye level ya max, usiweke batteries chini/sakafuni au kwenye tiles
Baada ya kusumbuka sana nilinunua zile betrii za mobisol huu mwaka wa tatu hakuna usumbufu.
 
Msaada na kwangu wakuu..... nna panel ya 150 na betri dry n100 ya gari nikitumia charger control inaonekana kujaa kabisa lakini ukija kuwasha hata balbu moja tu haichukui hata dk 20 imeisha chaji.... ila ukiunga direct ni masaa manne tu nawasha balbu tano usiku kucha...... zamani nilivyofunga hii system nlikuwa nikiangalia tv mchana kutwa na usiku kucha nawasha balbu nne..... je tatizo inaweza kuwa nini?
 
Controller. Ila hapo uliposema ukiunga DIRECT unamaanisha nini, kuunga Panel direct kwenye batteries? Ni hatari kama huna ulinzi, panel itaondoka kimasihara tu.

Na kama ni kuunganisha hizo balbu direct kwenye batteries, ndio unapata masaa 4 ila ukipitia controller ni dk 20, tafuta tu controller nyingine.
 
Shukraan mkuu.... kuunga kwa maana ya kuunganisha moja kwa moja toka panel mpaka betri bila kutumia controller
 
Shukraan mkuu.... kuunga kwa maana ya kuunganisha moja kwa moja toka panel mpaka betri bila kutumia controller
Utaunguza hizo photocells za kwenye panel yako, waya kupata joto n.k Panel yako inatoa Volts ngapi? 12, 24, 36 au 48? Tafuta Diode ya saizi stahiki ufunge kwenye waya mwekundu.
 
Angalia level ya maji kwa kila week au mara moja kwa mwezi, ongeza distilled water mpaka kwenye level ya max, usiweke batteries chini/sakafuni au kwenye tiles
Mkuu, hata kama battery imeandikwa 'regulated lead acid' inawekewa distilled water? Vipi nikiweka maji makali ya battery?
 
Naunganishaje tv na king'amzi (vyote ni dc)katika mfumo wa betri na charger controla ili viweze kuwaka? Naunga kwenye terminal za betri au kwenye output ya sola controla
 
Hakuna cha kujaribu, hiyo betri imekufa katupe au wauzie wanunua scraper Kama wapo. Betri nzuri ni dry za RITAR. Nunua N.100, solar panel watts100 halafu charge controller ya 10A, funga, hapo utacheka mpaka jino la mwisho lionekane. Ila usiogope gharama.
Nakubaliana na wewe betri nzuri dry ya ritar N100 mimi ninayo pia ina miaka mitatu lakini ndio inazidi kuwa strong, ila hapo kwenye solar panel umepuyanga, kioo cha watt100 hakina uwezo wa kujaza betri ya N100 kila siku Never. Hiyo betri itakuwa haijai, na at the end hiyo betri itakufa, kioo kinachoweza kujaza vizuri betri ya N100 ni kioo cha watt150, na hapo kwenye control 10amp ni ndogo inafaa 20amp. Yani ukifunga system yako kwa mpangilio huo maisha utayaona matamu sana. Nawasilisha
 
Naunganishaje tv na king'amzi (vyote ni dc)katika mfumo wa betri na charger controla ili viweze kuwaka? Naunga kwenye terminal za betri au kwenye output ya sola controla
Unachotakiwa kufanya unganisha waya kwenye betri terminals, halafu nunua twin socket kwisha kazi TV na kingamuzi vyote vitawaka
 
Mimi nina solar panel 200W. Nikinunua Battery ya 100W itaweza kujaa na kuwasha taa zangu 16? (4 zinawaka usiku mzima na 12 zinawaka mpaka saa 5 tu)
 
Mimi nina solar panel 200W. Nikinunua Battery ya 100W itaweza kujaa na kuwasha taa zangu 16? (4 zinawaka usiku mzima na 12 zinawaka mpaka saa 5 tu)
Hiyo panel kwa betri la n100 ni kutoitendea haki yake.
Kama una betri la n100 panel ya 120w inakutosha kabisa
 
Back
Top Bottom