Aisee. Hizo million 500 wangemaliza kwanza mradi wao wa kuweka pavements kwenye barabara zao za City Centre. Pavements za samora avenue zimechoka sana, ohio street haina kabisa pavements, na baadhi ya mitaa ya Uptown haina pavements. Wangemalizia huo mradi kwanza at least barabara zote hadi kufika Azikiwe street.
Ila mimi wachawa wa mama mtanisamehe
Hiv ni lini muliona Rais wetu akienda kukagua mradi flani, ofisi flani hata bila taarifa....mbona hata maagizo yake hayatekelezeki...mfano ni Magufuli bridge ya mwanza....alitoa deadline iwe mwezi wa pili..juzi naskia wanasema mwezi wa nne. Miradi ya BRT Dar iko slow mno hasa BRT 3. BRT 2 naskia wawekezaji wa mabasi wanakuja na kusepa..so mpaka sasa hakuna kampuni la maana ambalo litaendesha huu mradi.
SGR lot 3,4,5 hakuna kinachoendelea. Kule mwanza ndo kabisaa hakuna hata mkandarasi site.
Ujenzi wa mji wa Magufuli, barabara za mzunguko uko slow mno... Msalato Airport juzi kamati imekuta wizi wa hatari pesa za mradi zinaongezeka kila siku.
Ujenzi wa Bandari kavu ya kwala ulifikia wap? Mbona maroli hayaelekei huko. Tulitegemea hata kampuni kubwa kama DP world nk ziwe na crane zake huko tayari...ili treni za mizigo usiku ziwe zinaleta makontena yote pale kwanza na maroli yanachukulia mizigo pale.
Ni mara ngapi maroli yanaparamia watu kwenye barabara za dar...serikali ina mpango gani kusolve hili tatizo.
Serikali ingekuwa serious barabara ya kutoka hata pale kwala mpaka Morogoro ingeanza kutanuliwa haraka sana...
Sijawahi muona hata akiongelea hiyo miradi, kwa nini iko slow, solution ni nini, na wana mpango gani. Yaani sifa ni nyingi kuliko uhalisia huku kwa ground.
Mimi sio mwanasiasa. Ila tukiendelea na this style of leadership by 2030 tutakuwa tuko hapahapa na kaGDP below $100b, Hata per capita itazidi kushuka kufika hata 500 maana miradi ya kimkakati ambayo ingeweza kuongeza GDP inapewa kisogo na iko slow kulinganisha ukuaji wa population.