Please guys huu uchawa tuukemee naona muelekeo mbaya kabisa.
Mama yenu anayeza kupata kura na upendo bila hata uchawa wa kelele. Ikiwa kila anacholenga anakitimiza.
Mama amezungukwa na Controversy nyingi za uuzaji wa ardhi na rasmali na uwekezaji wa kuficha ficha mpaka unatia shaka.
Nidhamu ipo chini ya utendaji, vitu vipo slow.
Kama mna nia ya kumfanya mama apendwe telekeza vitu vyote kikamilifu.
Sio unafungua alafu unaingia mitini kuongeza kero. BRT ujenzi kusua sua huku jijini na barabara zimetifuliwa ni mambo gani haya?
Mkakati wa nishati safi ni mzuri naupongeza. Ila hampo serious kuwaza tozo kwenye nishati safi itakayofanya watu waditch hiyo nishati warudi kule kule.
Punguzia kodi kwenye gari za CNG muone zitajaa, Gesi ni yetu serikali badala ya kutolea mimacho tozo, si iangalie volume ya gesi wanayouza.
Hamjifunzi nchi za Uarabuni na Mafuta yao ikiwa wanauza kwao wenyewe mafuta cheap.
Narudia PUNGUZA UCHAWA, ONGEZEA KAZI NA UTEKELEZAJI.
ONDOA MACHAWA GOVERNMENT WEKA WATAALAMU.