Battle: Mwanza (The Rock City) Vs Arusha (A-Town/Chuga)

MENEJA WA TANROADS MWANZA: TANGU RAIS SAMIA AINGIE MADARAKANI KASI YA UTOAJI FEDHA KUHUDUMIA MIRADI IMEKUWA KUBWA

Na Mwandishi wetu, Sengerema

Tangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kuingia madarakani, mabadiliko makubwa yameonekana katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya ujenzi wa miundombinu jambo ambalo limechangiwa na utoaji wa fedha za utekelezaji wa miradi kwa wakati na hivyo kuchangia kasi ya utekekelezaji wa miradi kuongezeka.

Hayo yamesemwa Aprili 23, 2023 mkoani Mwanza na Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Mhandisi Pascal Ambrose akiongea na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa miradi mbalimbali ya ujenzi miundombinu mkoani humo.

Mhandisi Ambrose, akitolea mfano mradi ambao kasi yake ya utekelezaji imeongezeka tangu Rais Samia ingie madarakani ni pamoja na ujenzi wa daraja la Kigongo-Busisi ambapo ujenzi wake aliukuta ukiwa takriban asilimia 25 lakini sasa umefikia asilimia 72.

Akiongelea miradi iliyokamilika ndani ya Mkoa wa Mwanza , Mhandisi Ambrose amesema

"Tumekamilisha mradi wa ujenzi wa barabara ya kutoka Usagara hadi Kisesa KM 17, dhumuni la ujenzi wa barabara hii ilikuwa ni kupunguza msongamano ndani ya jiji la Mwanza"

Miradi mingine ni pamoja na mradi wa usanifu wa barabara ya Mwanangwa-Misasi-Salawe ambayo tayari imeshaanza kutengewa fedha na serikali ili ianze kujengwa kwa kiwango cha lami.

"Barabara ya Mwanza kuelekea Shinyanga tumeshafanyia usanifu wa kina ili kuijenga kwa njia nne kuanzia Mwanza hadi Mwanangwa, na kipande cha kutoka Mwanangwa hadi Shinyanga kitajengwa upya kwa njia mbili"

Akielezea mkakati wa kupunguza msongamano ndani ya jiji la Mwanza , Mhandisi Ambrose amesema

"Kwa ajili ya kuondoa msongamano katika jiji la Mwanza, tumeshaanza usanifu wa barabara ya kutoka Mwanza -Nyanguge kuelekea mpakani na Simiyu. Kipande cha Mwanza-Nyanguge tumekifanyia usanifu kwa ajili ya kujenga njia nne"

Aidha, kwa mwaka huu Mhandisi Ambrose amebainisha kuwa, wanatarajia kufanya usanifu wa kina wa barabara ya kutoka Usagara hadi mpakani mwa Geita ili iendane na upana wa daraja la Kigongo-Busisi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wazungu wanaendesha baiskeli kama mazoezi tambua hilo na pia ni jadi...Bora uwe mswahili kuliko mshamba.
 
Unyama sana boss
 
Porojo hizo Toka 2015 πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…