BATTLE: Vitu Original vs Vitu vya mtumba (used)

BATTLE: Vitu Original vs Vitu vya mtumba (used)

fizo talent

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2017
Posts
2,255
Reaction score
3,889
Habari wanajamvi
Km kichwa cha habari kinavyojieleza kumekuwapo na wimbi kubwa hususani ktk nchi yetu ya Tz ya biashara ya vitu vilivyotumika almaarufu kwa kwa jina la vitu vya mtumba ama vitu used,kwa upande wa vitu original (nimetumia neno original kwa kua sijapata kiswahili chake sanifu} hivi ni vitu vipya kabisa kimuonekano na hakikuwahi kutumika mahala popote.

Ktk nchi yetu soko la vitu vya mtumba ni kubwa kiasi ambacho limeenea ktk sekta mbalimbali mfano ni kwenye mavazi hapa unakutana na nguo na viatu,ukiangalia kwenye masuala ya umeme huko napo pamejaa majokofu,viyoyozi,tv,pasi,rice cooker yani huku ndio pamejaa na sehem mbalimbali tu pamejaa hivi vitu vya mtumba.
Soko limekua kubwa kiasi kwamba vitu vya mtumba vinasifiwa kua ni bora kuliko vitu original mfano mdogo ukienda dukani ukanunua jinz yako ya 25000 na mwingine akaenda zake ilala au karume na akapata jinz km yako kwa 15000 bac ww wa dukani unaonekana ni mshamba na umepigwa.
Ishu ni kwamba je ni kweli vitu vya mtumba ni bora kuliko original au ni upungufu wa kipato ndio unàotufanya tuamini kua vitu vya mtumba ni bora kuliko vitu original.
 
Hio orijino tunaita spesho

Enzi zileee za mwalimu tulikua tunaita redimedi

Ni uchumi wa mtu ndo unapelekea kupenda vitu spesho au mtumba.

Fikiria nguo za ndani za mtumba khaaa uchafu,mswaki wa mtumba etc

Kitu spesho kinaongeza hadhi ya mtu,kinapandisha heshima na kuonekana mtu mbele za watu hasa kwenye jamii zinazohukumu watu kwa mavazi ya gharama

Vifaa vya nyumban special vinapendezesha nyumba na vinadumu hasa ukinunua vile halisi.
 
Mkuu hebu fafanua kidogo. Orijino na mtumba. Una maanisha nini?
 
Ukiona jamii inaona ni bora kutumia mtumba kuliko kipya jua kuna tatizo(kama gharama sio kikwazo)
 
Back
Top Bottom