Batuli Actress aka Cleopatra Nabisha Hodi


Asante sana. Malkia ni yupi huyo?
 

Asante kwa maoni yako. Yatazingatiwa katika kazi zangu binafsi.

Kama nilivyoandika, jina la Movie zinategemea sana, Story Writer na Producer. Msanii kazi yangu ni kuigiza.

Sina uhakika na mambo ya part 1 & 2 maana hili liko kwa Distributors zaidi pia. Huenda limekaa Kibiashara zaidi.
 
Karibu jf but tunaomba mpunguze kuvaa nguo za nusu uchi...sisi tunataka kazi na si maungo yenu...waambie hao....maana nguo za club ndo wanazivaa kwenye shooting sijui ndo mauzo..mpk ney akawaamba makahaba wenye viwango wako bongo movie...achen

Asante. Umesomeka I hope Wasanii tutazingatia ushauri huu.
 
Mimi sio mtazamaji sana wa bongo movie na sijawahi tazama filamu uliyoigiza, lkn kwa vile umejiunga JF ngoja nitajidi nitazame kazi ulizofanya.

Karibu JF.
 
Hongera kwa kutumia really Username yako.
Japo Me nalionea ungetumia ID nyingine ili uweze kujua watu tunawachukuliaje nyie katika Jamii yetu ya KITANZANIA. Japo utaniuuliza kwani kwa kumia jina hili hutajua?
Utajua lakini sio kama ambavyo ungetumia Jina lingine, wapo watu wengine watasema kuwa wanakufagilia sana kumbe ni wanafiki tu. Kwa Mfano; Mtu ukianzisha Thread "Napenda sana anavyoigiza huyu msanii BATULI wengine watacomment hivi " Aaahhhhh!!!!!!! Yule ni Malaya wa kutupwa".

Yangu ni hayo tu, Karibu na karibia na Uwakaribishe wasanii wenzako ili nao wakaribie katika Jukwaa la The Greater Thinkers.
 

Asante sana. Kama nilivyosema nimejiunga JF kwa ajili ya kujifunza na pia kubadilishana mawazo. Changamoto zinaweza kuwepo na kwangu binafsi ni jambo la kawaida na zinaweza kunisaidia kujijenga zaidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…