BAVICHA: Tumesikitishwa sana na walioenda kuapa, ni kitendo cha usaliti, hujuma na hakiwezi kuvumilika. Wataka hatua kali zichukuliwe

BAVICHA: Tumesikitishwa sana na walioenda kuapa, ni kitendo cha usaliti, hujuma na hakiwezi kuvumilika. Wataka hatua kali zichukuliwe

Watumie hekima wawasamehe, waendelee kuwa wamoja.
Mbowe ana hekima sana, wanaweza kutumia busara kuwaacha waingie Bungeni huku jitihada nyingine za kudai haki zikiendelea. Nje ya busara watakisambaratisha chama.

Pia Rais ana nafasi nyingine 10 za viti maalum vya ubunge, anaweza kuwateua wapinzani wa kiume mfano Lisu, Mbatia, Myika na Mbowe natamani kusikia wakirudi bungeni.

Ustawi wa amani ya nchi ni muhimu sana kuliko kuwaza migogoro na kuiwekea nchi vikwazo, tutakaoumia ni wengi.
 
Leo baraza la vijana wa CHADEMA Taifa limetoa msimamo kufuatia wabunge 19 ambao wamekwenda kuapa bungeni kinyume na msimamo wa chama.

MWENYEKITI: BAVICHA tulikutana katika kikao chetu tulichokifanya kwa njia za kidijitali kujadili mustakabali wa chama chetu kufuatia kadhia hii iliyotokea katika chama.

Jambo la kwanza ambalo BAVICHA tumekubaliana ni kuunga mkono msimamo wa chama chetu, kwanza kutotambua matokeo ya uchaguzi, kutoutambua uchaguzi wote na matokeo yake yote. Huo msimamo wa kwanza ambao umekuwa ukitangazwa na chama chetu kuanzia mwanzo huo ndio msimamo wa BAVICHA.

Pili tunaunga mkono msimamo wa chama juu ya hawa ambao walienda kuapa, walioenda kinyume na muongozo wa chama chetu, tunaunga mkono msimamo wetu wa chama kwamba watu hawa waitwe hatua za kinidhamu ziweze kuchukuliwa dhidi yao.

Tunaunga mkono msimamo wa chama kwasababu kamati kuu ya CHADEMA ambayo ina uwakilishi wa vijana kwenye kamati hiyo na muwakilishi wa vijana hao ni mimi, katika vikao vya kamati kuu ya chama hatukuwahi kujadili, hatujawahi kupitisha orodha yoyote ya wabunge wa viti maalum.

Hatujawahi kujadili, hatujawahi kupitisha orodha yoyote ya wabunge wa viti maalum. Vijana wa CHADEMA tumekubaliana kuitaka tume ya uchaguzi ijitokeze hadharani iseme waziwazi orodha ya viti maalum ambayo tume inasema eti ni ya CHADEMA imetoka kwa nani katika mamlaka za chetu chetu.

Sisi kama BAVICHA kwanza tumesikitishwa sana na hawa watu walioenda kuapa, ni kitendo cha usaliti, hujuma na hakiwezi kuvumilika na taasisi yoyote na kwakuwa katibu mkuu amesema wanaruhusu maoni na mapendekezo ya wanachama ili chama kiweze kuchukua hatua, sisi kama kamati ya utendaji tumekaa na tumeamua kwa kauli moja tuishauri kamati kuu ya chama ichukue hatua kali za kinidhamu kwa watu hawa kwa ajili ya mustakabali wa chama chetu.

Hatua kali za kinidhamu zichukuliwe kwa ajili ya hawa 19 ambao walienda kuapa kama wabunge wa viti maalum, nitawakilisha mapendekezo hayo ya BAVICHA lakini kwa sasa tunaungana na wanachadema wote na watanzania ambao wanataka hawa watu 19 bila kujali nafasi, bila kujali wamefanya nini katika chama hiki lakini kwasababu ya usaliti huu lazima hatua za kinidhamu zichukuliwe na chama chetu.


Dar es Salaam. — AS the dust is settling after a general election that handed President John Magufuli a second term, life is going on in Tanzania with the ecstasy to the winners and disappointment to the losers giving way to the wisdom from an old adage that there is life after elections.

The election was not a magic wand to dispel social and economic complexities brought about notably by the outbreak of Covid-19.

 
Hallima Mdee na wenzake WAMELALA MAHABUSU na kudhalilika HAINA MFANO.....

Sikuona WAKIITWA WASALITI NA WANAFIKI....

Je akina MINYOO na genge lake...akina John Pambalu na genge lake ..akina Hilda NEWTON na genge lake.....SI WASALITI KWA KUTOTOKEA MAANDAMANONI pale UBUNGO?!!!!
 
Minyoo hakukanyaga UBUNGO walipoitisha maandamano akina MDEE leo ANATUKANA WATU kuwa ni WASALITI NA WANAFIKI....🤣🤣🤣🤣
 
Chadema ILICHANGISHA WATU kipindi cha kampeni za mwaka huu...

Najiuliza,watawezaje KUWALIPA MISHAHARA WAFANYAKAZI WAO huku hawapati RUZUKU?!!

WANATAKA WAFANYAKAZI WAO wawe wanajitolea kwa miaka 5....siasa gani hii?!!!

Hawa Ni wanaharakati ama wanasiasa?!!!
 
Hata mume au mke anaweza kusaliti akasamehewa kwa kupewa nafasi ya mwisho asirudie Tena, Sasa kina Mdee huwezi jua ni mazingira yapi walikutana nayo, pili Kama imetumika njia ya kuwagawa na mkaa mkasuruhishana mkayajenga upya kosa liko wapi? Au nilazima kubomoa tu hata Kama unaona taa nyekundu iliyotumika kufanyikisha hivyo? Mimi sijui Ila nadhani wakae wayamalize waendelee na ubunge pia kwa niaba ya 50/50 ya kuwainua wanawake duniani.
 
Kukosekana kwa RUZUKU baada ya kuwafukuza akina Hallima MDEE kutasababisha CHADEMA ipunguze WAFANYAKAZI wake INAOWALIPA....

Je WATAIMARIKA ZAIDI ama NDIO KUKIZIKA CHAMA CHAO?!!!
 
😜😜😜
Chadema haiishiwi majembe, kama huyo Mdee aliokotwa jalalani mwambieni ajue wataokotwa wengine wawe zaidi yake.

Chadema ni wapenzi na wanachama, sio hao wajuaji waliojiona wameota mapembe.
😜😜😜
 
Wasipowafukuza haraka ndipo watakuwa kama CUF ya Lipumba NCCR na TLP, lakini wakifukuzwa chadema itaheshimika kwa kuwa na misimamo thabiti na itaongeza wanachama zaidi na kuwa imara zaidi
Kuwafukuza kutaleta utata,Spika Ndugai atawakingia kifua.
Mdee sio mjinga atakiwasha,Chama kitagawanyika vipande,matokeo yake wataenda kortini. Majibu yapo wazi kama ilivyokuwa kwa CUF.

Lakini kibaya zaidi kitendo cha kuwafukuza mama wapambanaji kinaweza kutafsiriwa na European union kuwa ni mfumo dume na kitaungwa na wabunge wanawake walio bunge la Ulaya.

Mdee na wabunge wenzie waache waendelee kuwa wabunge.
 
Naunga mkono hoja wafukuzwe bila kupepesa macho kulinda credibility ya chama, ingawa taarifa za kiintelijensia zinaonyesha katika hilo kundi kuna waliotishwa , walioahidiwa, kuna waliofanyiwa ugaidi Nusrat Hanje na Salome Makamba kwa vitisho walivyopewa sijui kama watausema ukweli kwenye kamati kuu maana kufika kwao tu kwenye kamati kuu kunategemea Jiwe ameamkaje?

Amewaelekezaje? Dona kantri wanahangaikia kwelikweli tilioni mbili za LAAC na PAC, Kati ya heshima na msaada tutalinda heshimaaaa in Kabudi's voice hata mwezi haujaisha wanahangaika tilioni mbili?
 
Ila Halima ni mafia.. Kawatosa viherehere wote.. Wanasaga rumba na sisi huku mitaani.
 
Catherine Ruge unateseka sana dada

Pole sana najua ungekua kwenye list ungekua umepiga kimya....

Ha ha ha hawa watu ni vituko.

Tuliwaambia mteuliwa sio wakatutusi leo wanatukanana wao kwa wao.
 
Catherine Ruge unateseka sana dada

Pole sana najua ungekua kwenye list ungekua umepiga kimya...

Ha ha ha hawa watu ni vituko.

Tuliwaambia mteuliwa sio wakatutusi leo wanatukanana wao kwa wao.
 
Ila Halima ni mafia.. Kawatosa viherehere wote.. Wanasaga rumba na sisi huku mitaani.
.... alikuwa pandikizi ndani ya chama; hadi kufikia nafasi ya juu kabisa Mwenyekiti Bawacha - Taifa. Alikuwa kwenye payroll upande wa pili.
 
Catherine Ruge unateseka sana dada

Pole sana najua ungekua kwenye list ungekua umepiga kimya....

Ha ha ha hawa watu ni vituko.

Tuliwaambia mteuliwa sio wakatutusi leo wanatukanana wao kwa wao.
 
Back
Top Bottom