Uzalendo wa Kitanzania
JF-Expert Member
- Mar 8, 2020
- 3,585
- 8,106
Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha) limesema litakwenda mahakamani kufungua kesi iwapo wanawake 19 waliofukuzwa katika chama hicho wataendelea kutambulika kama wabunge wa Chadema.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma leo Jumamosi Aprili 24, 2021 mweka hazina wa Bawacha, Catherine Ruge amesema watachukua hatua hiyo iwapo wabunge hao wataendelea kuwepo bungeni na kwamba wapo tayari kuuthibitishia umma kuwa walifukuzwa Chadema.
Amesema wanamtaka Spika wa Bunge, Job Ndugai kujitokeza hadharani kuwaeleza Watanzania kama kweli ofisi ya Bunge haikupokea uthibitisho wa Chadema wabunge hao kufukuzwa uanachama.
"Hatutaendelea kuona katiba inaendelea kuvunjwa kwani ofisi ya Bunge inafahamu kwamba wabunge hao wamepoteza sifa za kuwa wabunge."
"Ni jambo la dharau kuona chama kinasema kimewavua ubunge wanachama wao eti naibu spika anakataa na kusema hana taarifa..., na si kweli kama Bunge halina taarifa ya kuvuliwa uanachama hao wanaoitwa wabunge wa Chadema hii ni dharau kubwa," amesema Catherine.