BAWACHA kuwapeleka Mahakamani wabunge 19 waliofutwa uanachama CHADEMA

Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha) limesema litakwenda mahakamani kufungua kesi iwapo wanawake 19 waliofukuzwa katika chama hicho wataendelea kutambulika kama wabunge wa Chadema.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma leo Jumamosi Aprili 24, 2021 mweka hazina wa Bawacha, Catherine Ruge amesema watachukua hatua hiyo iwapo wabunge hao wataendelea kuwepo bungeni na kwamba wapo tayari kuuthibitishia umma kuwa walifukuzwa Chadema.

Amesema wanamtaka Spika wa Bunge, Job Ndugai kujitokeza hadharani kuwaeleza Watanzania kama kweli ofisi ya Bunge haikupokea uthibitisho wa Chadema wabunge hao kufukuzwa uanachama.

"Hatutaendelea kuona katiba inaendelea kuvunjwa kwani ofisi ya Bunge inafahamu kwamba wabunge hao wamepoteza sifa za kuwa wabunge."

"Ni jambo la dharau kuona chama kinasema kimewavua ubunge wanachama wao eti naibu spika anakataa na kusema hana taarifa..., na si kweli kama Bunge halina taarifa ya kuvuliwa uanachama hao wanaoitwa wabunge wa Chadema hii ni dharau kubwa," amesema Catherine.
Ngoja tuone Ndugai atasemaje juu ya wabunge hawa ambao mimi ninawaita wabunge hewa!
 
Kabisa maana watatapakanya bil 16+ bure bure tu maana sio wabunge.
 
Mbona Halima alishasema "hili swala mbona dogo sana'. Watu wanatoka mishipa utafiri jambo kubwa!
 
ni kosa kubwa mno kuvunja Katiba ya Jamhuri. wapelekwe mahakamani ili haki itendeke.
 
Hakuna kwenda Mahakamani mpaka vikao vyote vya chama vitimize wajibu wake.

Mnyika na Mbowe acheni longolongo Itisheni Baraza kuu tusikilize rufaa za hao madada, Kinyume cha hapo sisi tutajua kuwa huu mchezo mnaucheza nyinyi huku mkituzuga!
😁😁 kweli nyumbu ni zero brain, yani mbaka saizi hamjui kwamba DJ anawabadilishia music tu mnademka kama wehu, mbaka mkijakushtuka mtajikuta kumbe mlikuwa mnademka bila nguo.

Mnaandika barua ya uteuzi, badae mnasema feki, mnaandika barua ya kuwatengua uanachama, hapohapo kwamsisitizo na lugha laiiiini, mnasema mnawaomba wakaterufaa, rufaa haijasikilizwa mnasema rais aingilie kati kuwatoa mara spika awatoe,then wakishinda rufaa what's gonna happen?, nyie watu mna kwama wapi.

Pambaneni na DJ, acheni kupoteza mda kutafuta huruma kwa spika na rais.

Mnaona mmepuuzwa na mama mnanza kutishia kwenda mahakamani!! ugoro mtupu.

Ndio mana Jembe alikuwa anawa tuliza mana mnaleta vi tantion uchwara visivyokuwa na mana.
 
Kwanini halmashauri kuu isikae na kupitia rufaa zao na kuhalalisha maamuzi ya kamati kuu?
Huu mchezo Chadema mnauchelewesha wenyewe.
Wakati RUFAA inakatwa, hukumu ya mwanzo ndiyo inakuwa active... Na ndo hasa walichokikat Rufaa...
 
Hakuna kwenda Mahakamani mpaka vikao vyote vya chama vitimize wajibu wake.

Mnyika na Mbowe acheni longolongo Itisheni Baraza kuu tusikilize rufaa za hao madada, Kinyume cha hapo sisi tutajua kuwa huu mchezo mnaucheza nyinyi huku mkituzuga!
Rufaa ya kitu gani kama wao bado ni wabunge!? Ni logic ndogo tu...
 
Ofisi ya Bunge ina kesi ya kujibu katika hili seke seke la wabunge wasio na vyama kuwamo bungeni.
 
Chadema kupitia viongozi wake wakuu wanalijua hili...wanafanya hivi kwa ajili ya maslai yao.

Chadema imejaa uhuni haswa huyo mbowe ndo muhuni kubwa lao.

Sent from my TECNO-J8 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom