BAWACHA kuwapeleka Mahakamani wabunge 19 waliofutwa uanachama CHADEMA

Fanyeni kazi zinalipa,acheni makida
 
Chadema ni chama cha kihuni,kila mtu anaongea
Hao wabunge wamekata rufaa kwenye baraza kuu,na rufaa yao haijasikilizwa,kihere here cha kwenda mahakani kinatoka wapi?
Serikali ya mwenda zake walikuwa wana wasubiri waitishe kikao cha halmashauri kuu wakamatwe wafunguliwe kesi za uhujumu uchumi.
Siri ika vuja ndio maana hicho kikao hakija itishwa. Huyo ndie hayati mnae msifia. Acheni Mungu aitwe Mungu.
 
Ccm watafanya uchaguzi mwezi huu mwishoni na nafasi ni ya Mama Samia. ila kwa bawacha wameitisha uchaguzi tatizo nafasi ya mwenyekiti wameweka kaimu mwenyekiti sio mwenyekiti kamili
Mwenyekiti ni mmoja wa watimuliwa,ndio maana kuna kaimu mwenyekiti uchaguzi ni mambo ya ndani ya chama usin'gan'ganie tu mwenyekiti yupo wapi, wale hawana sifa kuwepo bungeni hilo lipo wazi na samia hataki rongorongo.....
 
Aliyekuwa anawalinda kaondoka inabidi nao wajiuzulu na kuomba msamaha, warudishe pesa , pia watuambie ilikuaje mpaka wakaamua kuenda kuapa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanini halmashauri kuu isikae na kupitia rufaa zao na kuhalalisha maamuzi ya kamati kuu?
Huu mchezo Chadema mnauchelewesha wenyewe.
Naona tunachanganya mambo hapa, hawa wamefukuzwa uanachama wakakata rufaa. Kukata rufaa bado hakujawaondolea adhabu yao ya kufutwa uanachama. Sasa kinachoshangaza kwanini wapo bungeni wakati rufaa yao haijasikilizwa na wao kushinda?

Mtu anapokukumiwa na kukata rufaa hawezi kuachiwa awe uraiani kabla ya kushinda rufaa yake. Ataendelea kuitumikia adhabu hadi pale rufaa yake itakaposikilizwa . Kwa hiyo hao wanaoitwa wabunge hawana sifa ya kuwa wabunge na hawatakiwi kuwa bungeni kwani siyo wanachama wa CDM.

Kusikiliza rufaa yao mapema ni sawa kama kweli wangekuwa wanatumikia adhabu waliyopewa. Lakini wapo bungeni kwa mabavu tu ya spika na serikali. Hawatumikii adhabu waliyopewa na hawakwenda mahakamani kuomba zuio la adhabu yao. Wao walikata rufaa maana yake wanatambua adhabu yao lakini spika hatambui hiyo adhabu kinyume kabisa na katiba na akawaruhusu waendelee kuwa wabunge. Kwa mtazamo wangu sioni hata maana ya kusikiliza hiyo rufaa yao kwa sababu hakuna adhabu wanayotumikia.
 
Hapa ndipo napoamini andiko lililoandikwa kuwa
"Ole wake amtegemeaye mwanadamu kuwa kinga yake" Waliyemtegemea leo hawezi kuwasaidia tena
 
Sijui kwanini mpaka leo CHADEMA hawakuwa wamekwenda mahakamani?

Vitu vingine havihitaji nguvu
 
Reactions: BAK
Nimekuelewa...
 
Safi sana BAWACHA ✊🏾✊🏾✊🏾✊🏾✊🏾
 
Hata mimi nawashangaa sana na tangu January nilikuwa napigia debe hili bila mafanikio.
Ulikuwa ukiuliza hili swali unajibiwa kirahisi tu eti “sisi tulishawafukuza hao C19, hatuna time nao tena”

Kama ile barua ya kuwateua ni forged, ilitakiwa mpaka sasa kuwe na kesi mahakamani.
 
Chadema ni chama cha kihuni,kila mtu anaongea
Hao wabunge wamekata rufaa kwenye baraza kuu,na rufaa yao haijasikilizwa,kihere here cha kwenda mahakani kinatoka wapi?
Hiyo yote ni kubuy time mkuu!

Mbowe na Mnyika wanajua wanachokifanya! Kwani unafikiri wao hawataki hela?
 
Kwanini halmashauri kuu isikae na kupitia rufaa zao na kuhalalisha maamuzi ya kamati kuu?
Huu mchezo Chadema mnauchelewesha wenyewe.
Mkuu, wakikuelewa unitag please!
Nyumbu huwa hawaelewi kitu, sana sana ni kutimua mbio wakiwa wameinamisha vichwa basi.
 
Mbowe ndiye steering wa huu mchezo naona watu mpaka saiz wapo gizan
 
Kuna mtu au kundi la watu ndani ya chadema linanufaika na uwepo wa hao wanaoitwa covid19 bungeni,ndiyo maana wana hit the bush around, hawawezi kuwa straight kamwe.
 
Ulikuwa ukiuliza hili swali unajibiwa kirahisi tu eti “sisi tulishawafukuza hao C19, hatuna time nao tena”

Kama ile barua ya kuwateua ni forged, ilitakiwa mpaka sasa kuwe na kesi mahakamani.
Lilikuwa ni jibu sahihi kwa mtazamo wangu.
Barua ya kuwateuwa kama ilithibitika wameforge, basi adhabu ya kuwafukuza ilikuwa sahihi kuliko kwenda mahakamani. Ni adhabu ambayo kisheria iliwavua vyeo vyao vyote ikiwepo na huo ubunge waliojiteuwa wenyewe. Kulikuwa na haja gani tena ya kwenda mahakamani kama katiba ya nchi ingefuatwa?
Tatizo haliko CDM, liko kwa Spika na Mwendazake ambao waliamua kuikanyaga katiba ya nchi na kuruhusu watu wasio na chama kuwa wabunge.
 
Ruzuku ruzuku..chama kitajiendeshaje bila ruzuku.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Iyokesi wamefungua mahakama gani ya hapa Tanzania au The Haugue?
Kama hapa Tanzania basi wakumbuke kesi kama hiyo alifunguliwa Zito akiwa CDM nini kilitokea!
Wale Covid-19 inawauma sana Chadema.kumbukeni kesi za nyani msizipeleke kwa ngedere. mnajisumbua na kuumiza nafsi zenu bure.
Ndungai yupo anawachabo tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…