Bayern Munich vs Ajax Nairobi! Rais William Ruto Atangaza Ufunguzi Rasmi wa Uwanja wa Raila Odinga Januari 5!

Bayern Munich vs Ajax Nairobi! Rais William Ruto Atangaza Ufunguzi Rasmi wa Uwanja wa Raila Odinga Januari 5!

Ikariiah

JF-Expert Member
Joined
Jul 17, 2019
Posts
287
Reaction score
314
Rais William Ruto ametangaza kuwa uwanja mpya wa Raila Odinga International Stadium, uliojengwa katika eneo la Talanta Sports City jijini Nairobi, utafunguliwa rasmi Januari 5, 2027, huku mechi inayotarajiwa kuzikutanisha klabu za Bayern Munich ya Ujerumani na AFC Ajax ya Uholanzi ikiwa sehemu kuu ya tukio hilo.
2914.jpg


Tangazo hilo limetolewa jioni ya Jumatano, Oktoba 28, 2026, baada ya Ikulu kutoa taarifa kwamba rais angewasilisha ujumbe maalum kupitia mitandao yake rasmi ya kijamii.

Uwanja huo wenye uwezo wa kubeba watazamaji 60,000 umebuniwa kuwa na miundombinu ya kisasa, ikiwemo skyboxes 52 za kifahari, maeneo maalumu ya wageni waalikwa na vifaa vya kuandaa mashindano makubwa ya kimataifa. Uwanja huo pia unatarajiwa kuwa miongoni mwa vituo muhimu vya mashindano ya AFCON 2027 yatakayoandaliwa kwa ushirikiano na Tanzania na Uganda.

Aidha Rais Ruto ametangaza rasmi jina jipya la Talanta Stadium, ambayo sasa itajulikana kama Raila Amolo Odinga International Stadium, kwa heshima ya aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kenya, Raila Odinga.

Je, kuleta klabu kubwa za Ulaya kama Bayern Munich na Ajax nchini kutakuwa chachu ya kukuza soka la Kenya au mafanikio ya uwanja huu yatategemea zaidi namna utakavyotumiwa kukuza vipaji vya ndani?
 

Attachments

  • HVugNzMWMAAr6X0.jpg
    HVugNzMWMAAr6X0.jpg
    190 KB · Views: 8
  • HVuf8geW0AAXKjH.jpg
    HVuf8geW0AAXKjH.jpg
    148.8 KB · Views: 14
Back
Top Bottom